2 Samuel 3:35 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha, watu wote walikwenda kumshawishi Daudi ale mkate wakati ulipokuwa bado mchana. Lakini Daudi aliapa akawaambia, “Mungu na aniue ikiwa nitaonja mkate au kitu chochote hadi jua litakapotua.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha watu wote wakaja kumsihi Daudi ale chochote kulipokuwa bado mchana; lakini Daudi akaapa, akisema, “Mungu na aniadhibu vikali zaidi, nikionja mkate au kitu kingine chochote kabla ya jua kutua!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakaja na watu wote wamshurutishe Daudi kula chakula, ukalipo bado mchana; lakini Daudi akaapa, akasema Mungu anitendee vivyo, na kuzidi, nikionja mkate, au kingine cho chote kabla lichwapo jua.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha, watu wote walikwenda kumshawishi Daudi ale mkate wakati ulipokuwa bado mchana. Lakini Daudi aliapa akawaambia, “Mungu na aniue ikiwa nitaonja mkate au kitu chochote hadi jua litakapotua.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha watu wote wakaja kumsihi Daudi ale cho chote kulipokuwa kungali bado mchana; lakini Daudi akaapa, akisema, “Mungu na anishughulikie, tena kwa ukali, kama nikionja mkate au kitu kingine cho chote kabla ya jua kutua!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha watu wote wakaja kumsihi Daudi ale chochote kulipokuwa kungali bado mchana; lakini Daudi akaapa, akisema, “Mungu na anishughulikie, tena kwa ukali, kama nikionja mkate au kitu kingine chochote kabla ya jua kutua!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakaja na watu wote wamshurutishe Daudi kula chakula, kukiwa bado mchana; lakini Daudi akaapa, akasema Mungu anitendee vivyo hivyo, na kuzidi, nikionja mkate, au kingine chochote kabla ya jua kutua.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha, watu wote walikwenda kumshawishi Daudi ale mkate wakati ulipokuwa bado mchana. Lakini Daudi aliapa akawaambia, “Mungu na aniue ikiwa nitaonja mkate au kitu chochote hadi jua litakapotua.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watu wote walipokuja kumpa Dawidi chakula, mchana ungaliko, Dawidi akaapa kwamba: Mungu na anifanyizie hivi na kupita hivi, nikionja mkate au cho chote kingine kabla ya kuchwa kwa jua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakaja na watu wote wamshurutishe Daudi kula chakula, ukalipo bado mchana; lakini Daudi akaapa, akasema Mungu anitendee vivyo, na kuzidi, nikionja mkate, au kingine cho chote kabla lichwapo jua.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha, watu wote walikwenda kumusihi Daudi akule chakula wakati ulipokuwa bado muchana. Lakini Daudi aliapa akawaambia: “Mungu aniue ikiwa nitaonja chakula au kitu chochote mpaka jua litakapotua.”