2 Samuel 3:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mungu aniue ikiwa sitatekeleza yote ambayo Mwenyezi-Mungu alimwapia Daudi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mungu na amwadhibu Abneri vikali zaidi ikiwa sitafanya kwa ajili ya Daudi kile Mwenyezi Mungu alichomwahidi kwa kiapo,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mungu amfanyie Abneri vivyo, na kuzidi, nisipomtendea Daudi kama vile Bwana alivyomwapia;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mungu aniue ikiwa sitatekeleza yote ambayo Mwenyezi-Mungu alimwapia Daudi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mungu na amshughulikie Abneri, tena kwa ukali, ikiwa sitafanya kwa ajili ya Daudi kile BWANA alichomwahidi kwa kiapo,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mungu na amshughulikie Abneri, tena kwa ukali, ikiwa sitafanya kwa ajili ya Daudi kile bwana alichomwahidi kwa kiapo,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mungu amfanyie Abneri vivyo hivyo, na kuzidi, nisipomtendea Daudi kama vile BWANA alivyomwapia;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mungu aniue ikiwa sitatekeleza yote ambayo Mwenyezi-Mungu alimwapia Daudi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, Mungu na amfanyizie Abineri hivi na hivi, nisipomfanyizia Dawidi yaleyale, Bwana aliyoapa kumfanyizia!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mungu amfanyie Abneri vivyo, na kuzidi, nisipomtendea Daudi kama vile BWANA alivyomwapia;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mungu aniue ikiwa sitatimiza yote ambayo Yawe alimwapia Daudi.