2 Samuel 4:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yule mtu aliyekuja kuniambia kuwa Shauli amekufa, akidhani kuwa ananiletea habari njema, nilimkamata na kumwua huko. Hivyo ikawa ndiyo zawadi niliyompa kutokana na taarifa yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
yule mtu aliponiambia, ‘Sauli amekufa,’ akadhani ananiletea habari njema, nilimkamata, nikamuua huko Siklagi. Hiyo ndiyo zawadi niliyompa kwa ajili ya taarifa yake!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
mtu mmoja aliponiambia, akasema, Tazama, Sauli amekufa, akidhani ya kuwa ameleta habari njema, nalimshika, nikamwua, huko Siklagi, ndio ujira niliompa kwa habari zake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yule mtu aliyekuja kuniambia kuwa Shauli amekufa, akidhani kuwa ananiletea habari njema, nilimkamata na kumwua huko. Hivyo ikawa ndiyo zawadi niliyompa kutokana na taarifa yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
yule mtu aliponiambia, ‘Sauli amekufa,’ akadhani ananiletea habari njema, nilimkamata, nikamwua huko Siklagi. Hiyo ndiyo zawadi niliyompa kwa ajili ya taarifa yake!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
yule mtu aliponiambia, ‘Sauli amekufa,’ akadhani ananiletea habari njema, nilimkamata, nikamuua huko Siklagi. Hiyo ndiyo zawadi niliyompa kwa ajili ya taarifa yake!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
mtu mmoja aliponiambia, akasema, Tazama, Sauli amekufa, akidhani ya kuwa ameleta habari njema, nilimshika, nikamwua, huko Siklagi, ndio ujira niliompa kwa habari zake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yule mtu aliyekuja kuniambia kuwa Shauli amekufa, akidhani kuwa ananiletea habari njema, nilimkamata na kumwua huko. Hivyo ikawa ndiyo zawadi niliyompa kutokana na taarifa yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
nilimkamata yule aliyeniletea habari ya kwamba: Tazama, Sauli amekufa! Naye alijiwazia kuwa mwenye habari njema, lakini nikamwua huko Siklagi kuwa mshahara, niliompa wa habari zake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
mtu mmoja aliponiambia, akasema, Tazama, Sauli amekufa, akidhani ya kuwa ameleta habari njema, nalimshika, nikamwua, huko Siklagi, ndio ujira niliompa kwa habari zake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule mutu aliyekuja kuniambia kwamba Saulo amekufa, akizani kwamba ananiletea habari njema, nilimukamata na kumwua kule. Hivyo ikakuwa ndiyo zawadi niliyomupa kutokana na habari yake.