2 Samuel 4:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ishboshethi mwana wa Shauli, alikuwa na watu wawili waliokuwa viongozi wa kikosi cha uvamizi; mmoja aliitwa Baana na mwingine Rekabu. Hao walikuwa wana wa Rimoni, mtu wa kabila la Benyamini kutoka mji wa Be-erothi, (kwa maana Be-erothi pia ulikuwa mali ya kabila la Benyamini).
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi mwana wa Sauli alikuwa na watu wawili waliokuwa viongozi wa vikundi vya uvamizi. Mmoja aliitwa Baana na mwingine Rekabu, waliokuwa wana wa Rimoni, Mbeerothi, kutoka kabila la Benyamini. Beerothi alihesabiwa kuwa sehemu ya Benyamini,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na huyo mwana wa Sauli alikuwa na watu wawili, maakida wa vikosi; jina lake mmoja akiitwa Baana, na jina la wa pili Rekabu wana wa Rimoni, Mbeerothi, wa wana wa Benyamini; (kwa maana Beerothi umehesabiwa kuwa wa Benyamini;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ishboshethi mwana wa Shauli, alikuwa na watu wawili waliokuwa viongozi wa kikosi cha uvamizi; mmoja aliitwa Baana na mwingine Rekabu. Hao walikuwa wana wa Rimoni, mtu wa kabila la Benyamini kutoka mji wa Be-erothi, (kwa maana Be-erothi pia ulikuwa mali ya kabila la Benyamini).
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi mwana wa Sauli alikuwa na watu wawili ambao walikuwa viongozi wa vikundi vya uvamizi. Mmoja aliitwa Baana na mwingine Rekabu, waliokuwa wana wa Rimoni, Mbeerothi, kutoka kabila la Benyamini. Beerothi alihesabiwa kuwa sehemu ya Benyamini,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi mwana wa Sauli alikuwa na watu wawili waliokuwa viongozi wa vikundi vya uvamizi. Mmoja aliitwa Baana na mwingine Rekabu, waliokuwa wana wa Rimoni, Mbeerothi, kutoka kabila la Benyamini. Beerothi alihesabiwa kuwa sehemu ya Benyamini,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na huyo mwana wa Sauli alikuwa na watu wawili, viongozi wa vikosi; jina lake mmoja akiitwa Baana, na jina la wa pili Rekabu wana wa Rimoni, Mbeerothi, wa wana wa Benyamini; (kwa maana Beerothi umehesabiwa kuwa wa Benyamini;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ishboshethi mwana wa Shauli, alikuwa na watu wawili waliokuwa viongozi wa kikosi cha uvamizi; mmoja aliitwa Baana na mwingine Rekabu. Hao walikuwa wana wa Rimoni, mtu wa kabila la Benyamini kutoka mji wa Be-erothi, (kwa maana Be-erothi pia ulikuwa mali ya kabila la Benyamini).
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huyo mwana wa Sauli alikuwa na watu wawili waliokuwa wakuu wa vikosi, mmoja jina lake Baana, wa pili jina lake Rekabu, wana wa Rimoni wa Beroti waliokuwa wana wa Benyamini, kwani nchi ya Beroti ilihesabiwa kuwa ya Benyamini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na huyo mwana wa Sauli alikuwa na watu wawili, maakida wa vikosi; jina lake mmoja akiitwa Baana, na jina la wa pili Rekabu wana wa Rimoni, Mbeerothi, wa wana wa Benyamini; (kwa maana Beerothi umehesabiwa kuwa wa Benyamini;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mwana huyo wa Saulo alikuwa na watu wawili waliokuwa viongozi wa makundi yake ya waaskari. Mumoja aliitwa Bana na mwingine Rekabu. Hao walikuwa wana wa Rimoni, mutu wa kabila la Benjamina wa muji wa Beroti (kwa maana Beroti vilevile ulikuwa mali ya kabila la Benjamina).