2 Samuel 4:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yonathani mwana wa Shauli, alikuwa na mtoto aliyelemaa miguu yake yote miwili. Mtoto huyo aliitwa Mefiboshethi. Mefiboshethi alikuwa na umri wa miaka mitano habari za kifo cha Shauli na Yonathani ziliposikika kutoka Yezreeli. Yaya aliyekuwa anamtunza aliposikia kuwa Shauli na Yonathani wameuawa huko Yezreeli, alimchukua Mefiboshethi akakimbia naye. Lakini alipokuwa anakimbia kwa haraka mtoto huyo alianguka, naye akalemaa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
(Yonathani mwana wa Sauli alikuwa na mwana aliyekuwa mlemavu miguu yote miwili. Alikuwa na umri wa miaka mitano wakati habari kuhusu Sauli na Yonathani zilipofika kutoka Yezreeli. Yaya wake akambeba ili kukimbia, lakini yaya alipokuwa anaharakisha kuondoka, mtoto alianguka akawa kiwete. Jina lake aliitwa Mefiboshethi.)
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Yonathani, mwana wa Sauli alikuwa na mwana aliyekuwa na kilema cha miguu. Alikuwa amepata miaka mitano, habari za Sauli na Yonathani zilipofika Yezreeli, na yaya wake akamchukua akakimbia ikawa, alipokimbia kwa haraka, huyo mtoto akaanguka, akawa kilema. Na jina lake aliitwa Mefiboshethi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yonathani mwana wa Shauli, alikuwa na mtoto aliyelemaa miguu yake yote miwili. Mtoto huyo aliitwa Mefiboshethi. Mefiboshethi alikuwa na umri wa miaka mitano habari za kifo cha Shauli na Yonathani ziliposikika kutoka Yezreeli. Yaya aliyekuwa anamtunza aliposikia kuwa Shauli na Yonathani wameuawa huko Yezreeli, alimchukua Mefiboshethi akakimbia naye. Lakini alipokuwa anakimbia kwa haraka mtoto huyo alianguka, naye akalemaa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
(Yonathani mwana wa Sauli alikuwa na mwana aliyekuwa mlemavu miguu yote miwili. Alikuwa na miaka mitano wakati habari kuhusu Sauli na Yonathani zilipofika kutoka Yezreeli. Yaya wake akambeba ili kukimbia, lakini yaya alipokuwa anaharakisha kuondoka, mtoto alianguka akawa kiwete. Jina lake aliitwa Mefiboshethi.)
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
(Yonathani mwana wa Sauli alikuwa na mwana aliyekuwa mlemavu miguu yote miwili. Alikuwa na miaka mitano wakati habari kuhusu Sauli na Yonathani zilipofika kutoka Yezreeli. Yaya wake akambeba ili kukimbia, lakini yaya alipokuwa anaharakisha kuondoka, mtoto alianguka akawa kiwete. Jina lake aliitwa Mefiboshethi.)
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Yonathani, mwana wa Sauli alikuwa na mwana aliyekuwa na kilema cha miguu. Alikuwa na umri wa miaka mitano, habari za Sauli na Yonathani zilipofika Yezreeli, na yaya wake akamchukua akakimbia ikawa, alipokimbia kwa haraka, huyo mtoto akaanguka, akawa kilema. Na jina lake aliitwa Mefiboshethi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yonathani mwana wa Shauli, alikuwa na mtoto aliyelemaa miguu yake yote miwili. Mtoto huyo aliitwa Mefiboshethi. Mefiboshethi alikuwa na umri wa miaka mitano habari za kifo cha Shauli na Yonathani ziliposikika kutoka Yezreeli. Yaya aliyekuwa anamtunza aliposikia kuwa Shauli na Yonathani wameuawa huko Yezreeli, alimchukua Mefiboshethi akakimbia naye. Lakini alipokuwa anakimbia kwa haraka mtoto huyo alianguka, naye akalemaa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yonatani, mwana wa Sauli, alikuwa na mtoto mume aliyelemaa miguu yote miwili; huyu alikuwa mwenye miaka mitano, ile habari ya kufa kwao Sauli na Yonatani ilipofika kutoka Izireeli; hapo mlezi wake akamchukua, akimbie naye. Ikawa, alipojihimiza kukimbia, yule mtoto akaanguka, akakipata hicho kilema cha miguu, nalo jina lake Mefiboseti.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Yonathani, mwana wa Sauli alikuwa na mwana aliyekuwa na kilema cha miguu. Alikuwa amepata miaka mitano, habari za Sauli na Yonathani zilipofika Yezreeli, na yaya wake akamchukua akakimbia ikawa, alipokimbia kwa haraka, huyo mtoto akaanguka, akawa kilema. Na jina lake aliitwa Mefiboshethi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yonatani mwana wa Saulo alikuwa na mutoto aliyekuwa kilema wa miguu. Mutoto huyo aliitwa Mefiboseti. Mefiboseti alikuwa na umri wa miaka mitano wakati habari za kifo cha Saulo na Yonatani ziliposikilika kutoka Yezereheli. Kwa wakati ule, mulezi wake aliposikia kwamba Saulo na Yonatani waliuawa kule Yezereheli, akamukamata Mefiboseti na kukimbia naye. Lakini alipokuwa anakimbia kwa haraka, mutoto huyo alianguka na kuwa kilema.