2 Samuel 4:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Rekabu na Baana wana wa Rimoni Mbeerothi, wakaenda nyumbani kwa Ishboshethi. Walifika huko adhuhuri, Ishboshethi alipokuwa anapumzika nyumbani kwake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Rekabu na Baana, wana wa Rimoni Mbeerothi wakaenda nyumbani mwa Ish-Boshethi; walifika huko alipokuwa kwenye mapumziko yake ya mchana.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na wale wana wa Rimoni, Mbeerothi, Rekabu na Baana, wakaenda wakafika nyumbani kwa Ishboshethi, wakati wa hari ya mchana, alipokuwa akipumzika adhuhuri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Rekabu na Baana wana wa Rimoni Mbeerothi, wakaenda nyumbani kwa Ishboshethi. Walifika huko adhuhuri, Ishboshethi alipokuwa anapumzika nyumbani kwake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Rekabu na Baana, wana wa Rimoni Mbeerothi wakaenda nyumbani kwa Ish-Boshethi, nao walifika huko wakati alipokuwa kwenye mapumziko yake ya mchana.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Rekabu na Baana, wana wa Rimoni Mbeerothi wakaenda nyumbani kwa Ish-Boshethi, nao walifika huko wakati alipokuwa kwenye mapumziko yake ya mchana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na wale wana wa Rimoni, Mbeerothi, Rekabu na Baana, wakaenda wakafika nyumbani kwa Ishboshethi, wakati wa joto la mchana, alipokuwa akipumzika adhuhuri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Rekabu na Baana wana wa Rimoni Mbeerothi, wakaenda nyumbani kwa Ishboshethi. Walifika huko adhuhuri, Ishboshethi alipokuwa anapumzika nyumbani kwake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wale wana wa Rimoni wa Beroti, Rekabu na Baana, wakaenda; napo, jua la mchana lilipokuwa kali, wakaingia nyumbani mwa Isiboseti, naye alikuwa amelala kupumzikia mchana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na wale wana wa Rimoni, Mbeerothi, Rekabu na Baana, wakaenda wakafika nyumbani kwa Ishboshethi, wakati wa hari ya mchana, alipokuwa akipumzika adhuhuri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Rekabu na Bana wana wa Rimoni wa Beroti wakaenda kwa nyumba ya Isiboseti. Walifika kule wakati wa jua kali ya muchana, Isiboseti alipokuwa anapumzika mwake.