2 Samuel 4:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Waliingia nyumbani wakijifanya kana kwamba wanataka kuchukua ngano, wakamkuta Ishboshethi amelala kitandani mwake ndani ya chumba chake cha kulala, wakamchoma mkuki tumboni. Baada ya kumwua hivyo hao ndugu wawili walimkata kichwa wakatoroka wakiwa wamekichukua. Walipitia njia ya Araba, wakasafiri usiku kucha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakaingia kwenye chumba cha ndani kana kwamba wanachukua ngano, wakamchoma Ish-Boshethi mkuki tumboni. Ndipo Rekabu na Baana nduguye wakatoroka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakafikia kati ya nyumba, kana kwamba wanataka kuchukua ngano, wakampiga mkuki wa tumbo; kisha Rekabu na Baana nduguye wakakimbia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Waliingia nyumbani wakijifanya kana kwamba wanataka kuchukua ngano, wakamkuta Ishboshethi amelala kitandani mwake ndani ya chumba chake cha kulala, wakamchoma mkuki tumboni. Baada ya kumwua hivyo hao ndugu wawili walimkata kichwa wakatoroka wakiwa wamekichukua. Walipitia njia ya Araba, wakasafiri usiku kucha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakaingia kwenye chumba cha ndani kana kwamba wanachukua ngano, wakamchoma Ish-Boshethi mkuki wa tumboni. Ndipo Rekabu na Baana nduguye wakatoroka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakaingia kwenye chumba cha ndani kana kwamba wanachukua ngano, wakamchoma Ish-Boshethi mkuki wa tumboni. Ndipo Rekabu na Baana nduguye wakatoroka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakafikia kati ya nyumba, kana kwamba wanataka kuchukua ngano, wakampiga mkuki wa tumbo; kisha Rekabu na Baana nduguye wakakimbia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Waliingia nyumbani wakijifanya kana kwamba wanataka kuchukua ngano, wakamkuta Ishboshethi amelala kitandani mwake ndani ya chumba chake cha kulala, wakamchoma mkuki tumboni. Baada ya kumwua hivyo hao ndugu wawili walimkata kichwa wakatoroka wakiwa wamekichukua. Walipitia njia ya Araba, wakasafiri usiku kucha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao wakaingia mpaka katikati ya nyumba wakichukua ngano; ndipo, walipomchoma tumboni, kisha Rekabu na ndugu yake Baana wakakimbia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakafikia kati ya nyumba, kana kwamba wanataka kuchukua ngano, wakampiga mkuki wa tumbo; kisha Rekabu na Baana nduguye wakakimbia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Waliingia ndani ya nyumba wakijifanya sawa vile wanataka kukamata ngano, walimukuta Isiboseti amelala juu ya kitanda chake ndani ya chumba chake cha kulala, wakamuchoma mukuki katika tumbo. Kisha kumwua hivyo hao wandugu wawili walimukata kichwa wakatoroka wakikibeba. Walipitia njia ya Araba, wakasafiri usiku kucha.