2 Samuel 4:7 — Compare Translations

7 translations compared side by side

Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walikuwa wameingia ndani ya nyumba alipokuwa amelala kitandani chumbani kwake. Baada ya kumchoma mkuki na kumuua, walikata kichwa chake. Walikibeba na kutembea usiku kucha kwa njia ya Araba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi walipoingia katika ile nyumba, alipokuwa amelala kitandani mwake, katika chumba chake cha kulala, wakampiga, wakamwua, wakamkata kichwa, wakachukua kichwa chake, wakaenda zao kwa njia ya Araba usiku kucha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walikuwa wameingia ndani ya nyumba wakati alipokuwa amelala kitandani chumbani kwake. Baada ya kumchoma mkuki na kumwua, walikata kichwa chake. Wakiwa wamekichukua, walitembea usiku kucha kwa njia ya Araba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walikuwa wameingia ndani ya nyumba wakati alipokuwa amelala kitandani chumbani kwake. Baada ya kumchoma mkuki na kumuua, walikata kichwa chake. Wakiwa wamekichukua, walitembea usiku kucha kwa njia ya Araba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi walipoingia katika ile nyumba, alipokuwa amelala kitandani mwake, katika chumba chake cha kulala, wakampiga, wakamwua, wakamkata kichwa, wakachukua kichwa chake, wakaenda zao kwa njia ya Araba usiku kucha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Vilikuwa hivi: walipoingia nyumbani, yeye alikuwa amelala kitandani pake katika chumba cha kulalia; nao walipokwisha kumwua kwa kumchoma, wakamkata kichwa, wakakichukua kichwa chake, wakaenda zao na kushika njia ya jangwani usiku kucha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)