2 Samuel 4:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Halafu walichukua kichwa cha Ishboshethi na kumpelekea Daudi huko Hebroni. Nao wakamwambia mfalme Daudi, “Hiki ni kichwa cha Ishboshethi mwana wa Shauli ambaye ni adui yako, aliyekuwa anataka kuyaangamiza maisha yako. Mwenyezi-Mungu leo amekulipizia kisasi dhidi ya Shauli na wazawa wake.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakamletea Daudi kichwa cha Ish-Boshethi huko Hebroni, wakamwambia mfalme, “Hiki hapa kichwa cha Ish-Boshethi mwana wa Sauli, adui yako, aliyejaribu kukuua. Siku hii ya leo Mwenyezi Mungu amemlipizia kisasi mfalme bwana wangu dhidi ya Sauli na uzao wake.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakamletea Daudi kichwa cha Ishboshethi huko Hebroni, wakamwambia mfalme, Tazama, hiki ni kichwa cha Ishboshethi, mwana wa Sauli, adui yako, aliyekutafuta roho yako; Bwana amemlipia kisasi bwana wangu mfalme hivi leo, juu ya Sauli, na juu ya wazao wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Halafu walichukua kichwa cha Ishboshethi na kumpelekea Daudi huko Hebroni. Nao wakamwambia mfalme Daudi, “Hiki ni kichwa cha Ishboshethi mwana wa Shauli ambaye ni adui yako, aliyekuwa anataka kuyaangamiza maisha yako. Mwenyezi-Mungu leo amekulipizia kisasi dhidi ya Shauli na wazawa wake.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakamletea Daudi kichwa cha Ish-Boshethi huko Hebroni, wakamwambia mfalme, “Hiki hapa kichwa cha Ish-Boshethi mwana wa Sauli, adui yako, aliyejaribu kuondoa uhai wako. Siku hii ya leo BWANA amemlipia kisasi mfalme bwana wangu dhidi ya Sauli na mzao wake.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakamletea Daudi kichwa cha Ish-Boshethi huko Hebroni, wakamwambia mfalme, “Hiki hapa kichwa cha Ish-Boshethi mwana wa Sauli, adui yako, aliyejaribu kuondoa uhai wako. Siku hii ya leo bwana amemlipia kisasi mfalme bwana wangu dhidi ya Sauli na mzao wake.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakamletea Daudi kichwa cha Ishboshethi huko Hebroni, wakamwambia mfalme, Tazama, hiki ni kichwa cha Ishboshethi, mwana wa Sauli, adui yako, aliyekutafuta roho yako; BWANA amemlipia kisasi bwana wangu mfalme hivi leo, juu ya Sauli, na juu ya wazao wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Halafu walichukua kichwa cha Ishboshethi na kumpelekea Daudi huko Hebroni. Nao wakamwambia mfalme Daudi, “Hiki ni kichwa cha Ishboshethi mwana wa Shauli ambaye ni adui yako, aliyekuwa anataka kuyaangamiza maisha yako. Mwenyezi-Mungu leo amekulipizia kisasi dhidi ya Shauli na wazawa wake.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hicho kichwa cha Isiboseti wakakipeleka Heburoni kwa Dawidi, wakamwambia mfalme: Hiki ni kichwa cha Isiboseti, mwana wa Sauli, aliyekuwa mchukivu wako, aliyeitaka roho yako. Siku hii ya leo Bwana amempatia bwana wangu malipizi kwake Sauli na kwa kizazi chake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakamletea Daudi kichwa cha Ishboshethi huko Hebroni, wakamwambia mfalme, Tazama, hiki ni kichwa cha Ishboshethi, mwana wa Sauli, adui yako, aliyekutafuta roho yako; BWANA amemlipia kisasi bwana wangu mfalme hivi leo, juu ya Sauli, na juu ya wazao wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu walikamata kichwa cha Isiboseti na kumupelekea Daudi kule Hebroni. Nao wakamwambia mufalme Daudi: “Hiki ni kichwa cha Isiboseti mwana wa Saulo ambaye ni adui yako aliyekuwa anataka kuyaangamiza maisha yako. Yawe leo amekulipizia kisasi juu ya Saulo na wazao wake.”