2 Samuel 5:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo awali, Shauli alipokuwa mfalme wetu wewe ndiwe uliyewaongoza Waisraeli vitani, na Mwenyezi-Mungu alikuambia ‘Utakuwa mchungaji wa watu wangu Israeli na utakuwa mkuu juu ya Israeli.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Zamani, wakati Sauli alikuwa mfalme juu yetu, wewe ndiwe uliyeiongoza Israeli vitani. Naye Mwenyezi Mungu alikuambia, ‘Wewe utawachunga watu wangu Israeli, na utakuwa mtawala wao.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Zamani za kale, hapo Sauli alipokuwa mfalme juu yetu, wewe ndiwe uliyewaongoza Israeli watoke nje, na kuingia ndani. Naye Bwana akakuambia, Wewe utawalisha watu wangu Israeli, nawe utakuwa mkuu juu ya Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo awali, Shauli alipokuwa mfalme wetu wewe ndiwe uliyewaongoza Waisraeli vitani, na Mwenyezi-Mungu alikuambia ‘Utakuwa mchungaji wa watu wangu Israeli na utakuwa mkuu juu ya Israeli.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Zamani, wakati Sauli alipokuwa mfalme juu yetu, wewe ulikuwa ndiye uliyeongoza Israeli vitani. Naye BWANA akakuambia, ‘Utawachunga watu wangu Israeli, nawe utakuwa kiongozi wao.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Zamani, wakati Sauli alikuwa mfalme juu yetu, wewe ndiwe uliyeiongoza Israeli vitani. Naye bwana alikuambia, ‘Wewe utawachunga watu wangu Israeli, na utakuwa mtawala wao.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Zamani za kale, hapo Sauli alipokuwa mfalme juu yetu, wewe ndiwe uliyewaongoza Israeli wakitoka nje kwenda, na kurudi vitani. Naye BWANA akakuambia, Wewe utawalisha watu wangu Israeli, nawe utakuwa mkuu juu ya Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo awali, Shauli alipokuwa mfalme wetu wewe ndiwe uliyewaongoza Waisraeli vitani, na Mwenyezi-Mungu alikuambia ‘Utakuwa mchungaji wa watu wangu Israeli na utakuwa mkuu juu ya Israeli.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Napo hapo kale, Sauli alipokuwa mfalme wetu bado, aliyewaongoza Waisiraeli kwenda na kurudi vitani ni wewe, naye Bwana alikuambia: Wewe utawachunga walio ukoo wangu wa Waisiraeli, nawe wewe utawatawala Waisiraeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Zamani za kale, hapo Sauli alipokuwa mfalme juu yetu, wewe ndiwe uliyewaongoza Israeli watoke nje, na kuingia ndani. Naye BWANA akakuambia, Wewe utawalisha watu wangu Israeli, nawe utakuwa mkuu juu ya Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Zamani, Saulo alipokuwa mufalme wetu wewe ndiwe uliyewaongoza Waisraeli katika vita, na Yawe alikuambia: ‘Utakuwa muchungaji wa watu wangu Waisraeli; utakuwa mukubwa juu ya inchi ya Israeli.’ ”