2 Samuel 5:20 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Daudi akafika Baal-perasimu, na kuwashinda Wafilisti; halafu akasema, “Mwenyezi-Mungu amepita katikati ya adui zangu kama mafuriko ya maji yaendayo kasi.” Kwa hiyo mahali hapo pakaitwa Baal-perasimu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Daudi akaenda Baal-Perasimu, na huko akawashinda Wafilisti. Akasema, “Kama mafuriko yanavyofurika, Mwenyezi Mungu amewafurikia adui zangu mbele yangu.” Kwa hiyo mahali hapo pakaitwa Baal-Perasimu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Daudi akaja Baal-perasimu, naye Daudi akawapiga huko; akasema, Bwana amewafurikia adui zangu mbele yangu, kama mafuriko ya maji. Basi akapaita mahali pale Baal-perasimu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Daudi akafika Baal-perasimu, na kuwashinda Wafilisti; halafu akasema, “Mwenyezi-Mungu amepita katikati ya adui zangu kama mafuriko ya maji yaendayo kasi.” Kwa hiyo mahali hapo pakaitwa Baal-perasimu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Daudi akaenda mpaka Baal-Perasimu na huko akawashinda Wafilisti. Akasema, “Kama mafuriko yafurikavyo, BWANA amewafurikia adui zangu mbele yangu.” Kwa hiyo mahali hapo pakaitwa Baal-Perasimu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Daudi akaenda mpaka Baal-Perasimu, na huko akawashinda Wafilisti. Akasema, “Kama mafuriko yafurikavyo, bwana amewafurikia adui zangu mbele yangu.” Kwa hiyo mahali hapo pakaitwa Baal-Perasimu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Daudi akaja Baal-perasimu, naye Daudi akawapiga huko; akasema, BWANA amewafurikia adui zangu mbele yangu, kama mafuriko ya maji. Basi akapaita mahali pale Baal-perasimu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Daudi akafika Baal-perasimu, na kuwashinda Wafilisti; halafu akasema, “Mwenyezi-Mungu amepita katikati ya adui zangu kama mafuriko ya maji yaendayo kasi.” Kwa hiyo mahali hapo pakaitwa Baal-perasimu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Dawidi alipokuja Baali-Perasimu; Dawidi alipowapiga huko akasema: Bwana amewaatua adui zangu mbele yangu, kama maji yanavyoatua ukingo. Kwa sababu hii akapaita mahali pale jina lake Baali-Perasimu (Maatuko).
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Daudi akaja Baal-perasimu, naye Daudi akawapiga huko; akasema, BWANA amewafurikia adui zangu mbele yangu, kama mafuriko ya maji. Basi akapaita mahali pale Baal-perasimu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Daudi akafika Bali-Perasimu na kuwashinda Wafilistini. Halafu akasema: “Yawe amepita katikati ya waadui zangu kama mafuriko ya maji yanayoenda mbio.” Kwa hiyo pahali pale pakaitwa “Bwana Anayepita Katikati”.