2 Samuel 5:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baadaye mfalme na watu wake walikwenda Yerusalemu kuwashambulia Wayebusi waliokuwa wenyeji wa nchi hiyo. Lakini wao wakamwambia, “Hutaingia mjini humu, kwani vipofu na vilema watakufukuzia mbali.” Walimwambia hivyo kwani walifikiri kuwa Daudi asingeweza kuingia mjini humo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme na watu wake wakaenda Yerusalemu kuwashambulia Wayebusi walioishi humo. Wayebusi wakamwambia Daudi, “Wewe hutaingia humu, kwani hata vipofu na viwete wanaweza kukufukuza.” Walidhani, “Daudi hawezi kuingia humu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha mfalme na watu wake wakaenda Yerusalemu ili kupigana na Wayebusi, wenyeji wa nchi ile; hao ndio waliomwambia Daudi, wakisema, Usipowaondoa vipofu, na viwete, hutaingia humu kamwe; huku wakidhania ya kuwa Daudi hawezi kuingia humo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baadaye mfalme na watu wake walikwenda Yerusalemu kuwashambulia Wayebusi waliokuwa wenyeji wa nchi hiyo. Lakini wao wakamwambia, “Hutaingia mjini humu, kwani vipofu na vilema watakufukuzia mbali.” Walimwambia hivyo kwani walifikiri kuwa Daudi asingeweza kuingia mjini humo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme na watu wake wakaenda Yerusalemu kuwashambulia Wayebusi walioishi huko. Wayebusi wakamwambia Daudi, “Hutaingia hapa ndani, kwani hata vipofu na viwete wanaweza kukufukuza.” Walidhani, “Daudi hawezi kuingia humu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme na watu wake wakaenda Yerusalemu kuwashambulia Wayebusi walioishi humo. Wayebusi wakamwambia Daudi, “Wewe hutaingia humu, kwani hata vipofu na viwete wanaweza kukufukuza.” Walidhani, “Daudi hawezi kuingia humu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha mfalme na watu wake wakaenda Yerusalemu ili kupigana na Wayebusi, wenyeji wa nchi ile; nao wakamwambia Daudi, hutaingia humu kamwe; maana hata vipofu na viwete watakufukuzia mbali; huku wakidhania ya kuwa Daudi hawezi kuingia humo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baadaye mfalme na watu wake walikwenda Yerusalemu kuwashambulia Wayebusi waliokuwa wenyeji wa nchi hiyo. Lakini wao wakamwambia, “Hutaingia mjini humu, kwani vipofu na vilema watakufukuzia mbali.” Walimwambia hivyo kwani walifikiri kuwa Daudi asingeweza kuingia mjini humo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha mfalme na watu wake wakaenda Yerusalemu kwa Wayebusi waliokuwa bado wenyeji wa nchi hiyo, nao wakamwambia Dawidi kwamba: Humu hutaiangia kabisa usipowaondoa vipofu na viwete, ni kwamba: Dawidi hataingia humu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha mfalme na watu wake wakaenda Yerusalemu ili kupigana na Wayebusi, wenyeji wa nchi ile; hao ndio waliomwambia Daudi, wakisema, Usipowaondoa vipofu, na viwete, hutaingia humu kamwe; huku wakidhania ya kuwa Daudi hawezi kuingia humo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha mufalme na watu wake walikwenda Yerusalema kuwashambulia Wayebusi waliokuwa wenyeji wa inchi hiyo. Lakini wao wakamwambia: “Hautaingia ndani ya muji huu, maana vipofu na vilema watakufukuza.” Walimwambia hivyo maana walifikiri kwamba Daudi asingeweza kuingia katika muji ule.