2 Samuel 6:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wale waliolibeba sanduku la Mwenyezi-Mungu kila walipopiga hatua sita, Daudi alitoa tambiko: Fahali na ndama mmoja mnono.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale waliokuwa wamebeba Sanduku la Mwenyezi Mungu walipotembea hatua sita, Daudi alitoa dhabihu fahali na ndama aliyenoneshwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata ikawa, watu waliolichukua sanduku la Bwana walipokwisha kwenda hatua sita, akachinja ng'ombe na kinono.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wale waliolibeba sanduku la Mwenyezi-Mungu kila walipopiga hatua sita, Daudi alitoa tambiko: fahali na ndama mmoja mnono.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wale waliokuwa wamebeba Sanduku la BWANA walipokuwa wametembea hatua sita, Daudi alitoa dhabihu fahali na ndama aliyenona.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wale waliokuwa wamebeba Sanduku la bwana walipokuwa wametembea hatua sita, Daudi alitoa dhabihu fahali na ndama aliyenoneshwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata ikawa, watu waliolichukua sanduku la BWANA walipokwisha kwenda hatua sita, akachinja fahali na ndama mnono.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wale waliolibeba sanduku la Mwenyezi-Mungu kila walipopiga hatua sita, Daudi alitoa tambiko: Fahali na ndama mmoja mnono.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa, wao wachukuzi wa Sanduku la Bwana walipokwisha kwenda hatua sita, akachinja ng'ombe ya tambiko na ndama aliyenona.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata ikawa, watu waliolichukua sanduku la BWANA walipokwisha kwenda hatua sita, akachinja ng’ombe na kinono.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wale waliolibeba Sanduku la Yawe kila mara walipopiga hatua sita, Daudi alitoa sadaka: ngombe dume na mwana-ngombe mumoja wenye kunona.