2 Samuel 6:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha waliliingiza sanduku la Mwenyezi-Mungu ndani ya hema ambalo Daudi alikuwa amelipiga hapo na kuliweka mahali pake. Naye Daudi akatoa tambiko za kuteketezwa na tambiko za amani mbele ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakaleta Sanduku la Mwenyezi Mungu na kuliweka mahali pake ndani ya hema ambalo Daudi alikuwa amelisimamisha kwa ajili yake, naye Daudi akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakaliingiza sanduku la Bwana, na kuliweka mahali pake, katikati ya hema aliyoipiga Daudi kwa ajili yake, naye Daudi akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha waliliingiza sanduku la Mwenyezi-Mungu ndani ya hema ambalo Daudi alikuwa amelipiga hapo na kuliweka mahali pake. Naye Daudi akatoa tambiko za kuteketezwa na tambiko za amani mbele ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakaleta Sanduku la BWANA na kuliweka mahali pake ndani ya hema ambalo Daudi alikuwa amelisimika kwa ajili yake, naye Daudi akatoa sadaka za kuteketezwa kwa moto na sadaka za amani mbele za BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakaleta Sanduku la bwana na kuliweka mahali pake ndani ya hema ambalo Daudi alikuwa amelisimamisha kwa ajili yake, naye Daudi akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakaliingiza sanduku la BWANA, na kuliweka mahali pake, katikati ya hema aliyoipiga Daudi kwa ajili yake, naye Daudi akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha waliliingiza sanduku la Mwenyezi-Mungu ndani ya hema ambalo Daudi alikuwa amelipiga hapo na kuliweka mahali pake. Naye Daudi akatoa tambiko za kuteketezwa na tambiko za amani mbele ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walipokwisha kuliingiza Sanduku la Bwana wakaliweka mahali pake katikati ya lile hema, Dawidi alilolipigia. Kisha Dawidi akamtolea Bwana ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima na za kumshukuru.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakaliingiza sanduku la BWANA, na kuliweka mahali pake, katikati ya hema aliyoipiga Daudi kwa ajili yake, naye Daudi akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha waliliingiza Sanduku la Yawe ndani ya hema ambalo Daudi alikuwa amelisimamisha pale na kuliweka pahali pake. Naye Daudi akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele ya Yawe.