2 Samuel 6:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Daudi aliondoka akaenda pamoja na watu wake wote aliokuwa nao kutoka Baala-yuda, kwenda kulichukua toka huko sanduku la Mungu linaloitwa kwa jina lake Mwenyezi-Mungu wa Majeshi, akaaye kwenye kiti chake cha enzi juu ya viumbe wenye mabawa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yeye na watu wake wote wakatoka Baala ya Yuda kulipandisha Sanduku la Mungu kutoka huko, linaloitwa kwa Jina, naam, jina la Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, anayeketi kwenye kiti cha enzi kati ya makerubi walio juu ya hilo Sanduku.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaondoka Daudi akaenda pamoja na watu wote waliokuwa naye, mpaka Baala wa Yuda, ili kulipandisha kutoka huko sanduku la Mungu lililoitwa kwa jina, naam, jina la Bwana wa majeshi akaaye juu ya makerubi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Daudi aliondoka akaenda pamoja na watu wake wote aliokuwa nao kutoka Baala-yuda, kwenda kulichukua toka huko sanduku la Mungu linaloitwa kwa jina lake Mwenyezi-Mungu wa Majeshi, akaaye kwenye kiti chake cha enzi juu ya viumbe wenye mabawa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yeye na watu wake wote wakatoka Baala ya Yuda kuleta kutoka huko Sanduku la Mungu, linaloitwa kwa Jina, naam, jina la BWANA Mwenye Nguvu Zote, ambaye ameketi kwenye kiti cha enzi kati ya makerubi walioko juu ya hilo Sanduku.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yeye na watu wake wote wakatoka Baala ya Yuda kulipandisha Sanduku la Mungu kutoka huko, linaloitwa kwa Jina, naam, jina la bwana Mwenye Nguvu Zote, ambaye anaketi katika kiti cha enzi kati ya makerubi walioko juu ya hilo Sanduku.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akaondoka Daudi akaenda pamoja na watu wote waliokuwa naye, mpaka Baala wa Yuda, ili kulipandisha kutoka huko sanduku la Mungu lililoitwa kwa jina, naam, jina la BWANA wa majeshi akaaye juu ya makerubi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Daudi aliondoka akaenda pamoja na watu wake wote aliokuwa nao kutoka Baala-yuda, kwenda kulichukua toka huko sanduku la Mungu linaloitwa kwa jina lake Mwenyezi-Mungu wa Majeshi, akaaye kwenye kiti chake cha enzi juu ya viumbe wenye mabawa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Dawidi akaondoka, akaenda nao hao watu wote waliokuwa naye kwenda Bale wa Yuda kulichukua huko Sanduku la Mungu lililoitwa jina lake kwa Jina la Bwana Mwenye vikosi akaaye juu ya Makerubi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaondoka Daudi akaenda pamoja na watu wote waliokuwa naye, mpaka Baala wa Yuda, ili kulipandisha kutoka huko sanduku la Mungu lililoitwa kwa jina, naam, jina la BWANA wa majeshi akaaye juu ya makerubi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Daudi aliondoka pamoja nao wote kuenda Bali-Yuda kwa kuleta Sanduku la Mungu linaloitwa kwa jina la Yawe wa majeshi, anayeikaa kwenye kiti chake cha kifalme juu ya makerubi.