2 Samuel 6:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Daudi akamwambia Mikali, “Nilikuwa mbele ya Mwenyezi-Mungu ambaye alinichagua mimi badala ya baba yako, na jamaa yake, ili kuniteua kuwa mkuu juu ya Israeli, watu wake Mwenyezi-Mungu, kwa hiyo mimi nitacheza tu mbele ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Daudi akamwambia Mikali, “Nilifanya hivyo mbele za Mwenyezi Mungu ambaye alinichagua mimi badala ya baba yako au mwingine yeyote kutoka nyumba yake aliponiweka niwe mtawala wa Israeli, watu wa Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo nitacheza mbele za Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Daudi akamwambia Mikali, Ilikuwa mbele za Bwana, aliyenichagua mimi juu ya baba yako, na juu ya nyumba yake, ili kuniweka niwe mkuu juu ya watu wa Bwana, juu ya Israeli; kwa hiyo mimi nitacheza mbele za Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Daudi akamwambia Mikali, “Nilikuwa mbele ya Mwenyezi-Mungu ambaye alinichagua mimi badala ya baba yako, na jamaa yake, ili kuniteua kuwa mkuu juu ya Israeli, watu wake Mwenyezi-Mungu, kwa hiyo mimi nitacheza tu mbele ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Daudi akamwambia Mikali, “Nilifanya hivyo mbele za BWANA ambaye alinichagua mimi badala ya baba yako au mwingine ye yote kutoka katika nyumba yake wakati aliponiweka niwe mtawala juu ya Israeli, watu wa BWANA. Kwa hiyo nitacheza mbele za BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Daudi akamwambia Mikali, “Nilifanya hivyo mbele za bwana ambaye alinichagua mimi badala ya baba yako au mwingine yeyote kutoka nyumba yake wakati aliponiweka niwe mtawala juu ya Israeli, watu wa bwana. Kwa hiyo nitacheza mbele za bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Daudi akamwambia Mikali, Nilikuwa mbele za BWANA, aliyenichagua mimi juu ya baba yako, na juu ya nyumba yake, ili kuniweka niwe mkuu juu ya watu wa BWANA, juu ya Israeli; kwa hiyo mimi nitacheza mbele za BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Daudi akamwambia Mikali, “Nilikuwa mbele ya Mwenyezi-Mungu ambaye alinichagua mimi badala ya baba yako, na jamaa yake, ili kuniteua kuwa mkuu juu ya Israeli, watu wake Mwenyezi-Mungu, kwa hiyo mimi nitacheza tu mbele ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Dawidi akamwambia Mikali: Bwana ndiye aliyenichagua na kumwacha baba yako na mlango wake wote, aliponiagiza mimi kuwa mkuu wao walio ukoo wake Bwana nao wao Waisiraeli, naye yeye Bwana ndiye, ambaye ninataka kucheza mbele yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Daudi akamwambia Mikali, Ilikuwa mbele za BWANA, aliyenichagua mimi juu ya baba yako, na juu ya nyumba yake, ili kuniweka niwe mkuu juu ya watu wa BWANA, juu ya Israeli; kwa hiyo mimi nitacheza mbele za BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Daudi akamwambia Mikali: “Nilikuwa mbele ya Yawe ambaye alinichagua mimi pahali pa baba yako na jamaa yake, kwa kunichagua kuwa mukubwa juu ya Waisraeli, watu wa Yawe. Kwa hiyo mimi nitacheza tu mbele ya Yawe.