2 Samuel 7:19 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena jambo hili lilikuwa dogo machoni pako, Bwana Mungu; zaidi ya hayo umeiahidi jamaa yangu mambo makubwa katika miaka mingi ijayo; na kwamba umenijalia kuona hayo, Ee Bwana Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Naam, kana kwamba hili halitoshi machoni pako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi, wewe umenena pia kuhusu siku zijazo za nyumba ya mtumishi wako. Je, hii ndiyo njia yako ya kawaida ya kushughulika na mwanadamu, Ee Bwana Mungu Mwenyezi?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena jambo hili lilikuwa dogo machoni pako, Ee Bwana MUNGU; hata umeleta habari ya nyumba yangu mimi, mtumwa wako, kwa miaka mingi inayokuja baadaye; na hayo kwa namna ya kibinadamu, Ee Bwana MUNGU.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena jambo hili lilikuwa dogo machoni pako, Bwana Mungu; zaidi ya hayo umeiahidi jamaa yangu mambo makubwa katika miaka mingi ijayo; na kwamba umenijalia kuona hayo, Ee Bwana Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Naam, kana kwamba hili halitoshi machoni pako, Ee BWANA Mwenyezi, wewe umenena pia habari za wakati ujao kuhusu nyumba ya mtumishi wako. Je, hii ndiyo njia yako ya kawaida ya kushughulika na mwanadamu, Ee BWANA Mwenyezi?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Naam, kana kwamba hili halitoshi machoni pako, Ee bwana Mwenyezi, wewe umenena pia kuhusu siku zijazo za nyumba ya mtumishi wako. Je, hii ndiyo njia yako ya kawaida ya kushughulika na mwanadamu, Ee bwana Mwenyezi?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena jambo hili lilikuwa dogo machoni pako, Ee Bwana MUNGU; hata umeleta habari ya nyumba yangu mimi, mtumishi wako, kwa miaka mingi inayokuja baadaye; na hayo kwa namna ya kibinadamu, Ee Bwana MUNGU.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tena jambo hili lilikuwa dogo machoni pako, Bwana Mungu; zaidi ya hayo umeiahidi jamaa yangu mambo makubwa katika miaka mingi ijayo; na kwamba umenijalia kuona hayo, Ee Bwana Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini hayo yakawa madogo machoni pako, Bwana Mungu, kwa hiyo umeyasema yatakayoujia mlango wa mtumishi wako katika siku zilizo mbali bado, hayo nayo umeyasema kimtu, Bwana Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena jambo hili lilikuwa dogo machoni pako, Ee Bwana MUNGU; hata umeleta habari ya nyumba yangu mimi, mtumwa wako, kwa miaka mingi inayokuja baadaye; na hayo kwa namna ya kibinadamu, Ee Bwana MUNGU.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena jambo hili lilikuwa dogo mbele ya macho yako. Zaidi ya hayo, Bwana wangu Yawe, umeahidi kuchunga jamaa yangu kwa miaka mingi inayokuja na kunijulisha hivyo, ee Bwana wangu Yawe.