2 Samuel 7:23 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena ni watu gani duniani ambao wanaweza kufananishwa na watu wako wa Israeli, ambao Mungu wake alikwenda kuwakomboa ili wawe watu wake? Wewe ee Mungu ulijifanyia jina na kujitendea mambo makubwa na ya ajabu kwa ajili ya nchi yako mbele ya watu wako ambao kwa ajili yako mwenyewe uliwaokoa kutoka Misri, ukayafukuza mataifa na miungu yake mbele yao?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Naye ni nani aliye kama watu wako Israeli, taifa pekee duniani ambalo Mungu alitoka kwenda kulikomboa kwa ajili yake mwenyewe, na kujifanyia jina mwenyewe, kwa kufanya maajabu makubwa na ya kutisha kwa kuwafukuza mataifa na miungu yao mbele ya watu wako, ambao uliwakomboa kutoka Misri?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena ni taifa lipi duniani lililo kama watu wako, kama Israeli, ambalo Mungu alikwenda kuwakomboa kwa ajili yake, wawe watu wake mwenyewe, akajifanyie jina, na kutenda mambo makuu kwa ajili yenu, na mambo ya kuogofya kwa ajili ya nchi yako, mbele ya watu wako, uliowakomboa kutoka Misri wawe wako, kutoka katika mataifa na miungu yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena ni watu gani duniani ambao wanaweza kufananishwa na watu wako wa Israeli, ambao Mungu wake alikwenda kuwakomboa ili wawe watu wake? Wewe ee Mungu ulijifanyia jina na kujitendea mambo makubwa na ya ajabu kwa ajili ya nchi yako mbele ya watu wako ambao kwa ajili yako mwenyewe uliwaokoa kutoka Misri, ukayafukuza mataifa na miungu yake mbele yao?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ni nani aliye kama watu wako Israeli, taifa pekee duniani ambalo Mungu alitoka kwenda kulikomboa kuwa taifa kwa ajili yake mwenyewe na kujifanyia jina mwenyewe na kufanya mambo makuu na maajabu ya kutisha kwa kuwafukuza mataifa na miungu yao kutoka mbele ya watu wako, ambao uliwakomboa kutoka Misri?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Naye ni nani aliye kama watu wako Israeli, taifa pekee duniani ambalo Mungu alitoka kwenda kulikomboa kwa ajili yake mwenyewe, na kujifanyia jina mwenyewe, kwa kufanya maajabu makubwa na ya kutisha kwa kuwafukuza mataifa na miungu yao mbele ya watu wako, ambao uliwakomboa kutoka Misri?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena ni taifa lipi duniani lililo kama watu wako, kama Israeli, ambalo Mungu alikwenda kuwakomboa kwa ajili yake, wawe watu wake mwenyewe, akajifanyie jina, na kutenda mambo makuu kwa ajili yenu, na mambo ya kuogofya kwa ajili ya nchi yako, mbele ya watu wako, uliowakomboa kutoka Misri wawe wako, kutoka katika mataifa na miungu yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tena ni watu gani duniani ambao wanaweza kufananishwa na watu wako wa Israeli, ambao Mungu wake alikwenda kuwakomboa ili wawe watu wake? Wewe ee Mungu ulijifanyia jina na kujitendea mambo makubwa na ya ajabu kwa ajili ya nchi yako mbele ya watu wako ambao kwa ajili yako mwenyewe uliwaokoa kutoka Misri, ukayafukuza mataifa na miungu yake mbele yao?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena liko taifa moja tu huku nchini linalofanana na ukoo wako wa Waisiraeli? Hao ndio, Mungu aliokwenda kuwakomboa, wawe ukoo wake, ajipatie Jina kwa kufanya kwao katika nchi yako matendo makubwa yanayoogopesha, ulipofukuza wamizimu na miungu yao mbele yao walio ukoo wako, uliowakomboa, wawe wako, ulipowatoa huko Misri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena ni taifa lipi duniani lililo kama watu wako, kama Israeli, ambalo Mungu alikwenda kuwakomboa kwa ajili yake, wawe watu wake mwenyewe, akajifanyie jina, na kutenda mambo makuu kwa ajili yenu, na mambo ya kuogofya kwa ajili ya nchi yako, mbele ya watu wako, uliowakomboa kutoka Misri wawe wako, kutoka katika mataifa na miungu yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena, hakuna watu katika dunia ambao wanaweza kufananishwa na watu wako Waisraeli. Ulikwenda kuwakomboa kutoka Misri na miungu yake kusudi wakuwe watu wako. Ukawafanyia jina na kuwatendea mambo makubwa na ya ajabu.