2 Samuel 7:27 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana wewe, ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, umenifunulia mimi mtumishi wako, ukisema ‘Nitakujengea nyumba;’ ndio maana nina ujasiri kutoa ombi hili mbele yako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli, umelifunua hili kwa mtumishi wako, ukisema, ‘Nitakujengea nyumba.’ Hivyo mtumishi wako amepata ujasiri kukuletea dua hili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa wewe, Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli umenifunulia mimi, mtumwa wako, ukisema, Nitakujengea nyumba; kwa hiyo mimi, mtumwa wako, nimeona vema moyoni mwangu nikuombe dua hii.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana wewe, ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, umenifunulia mimi mtumishi wako, ukisema ‘Nitakujengea nyumba;’ ndio maana nina ujasiri kutoa ombi hili mbele yako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ee BWANA Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, umelifunua hili kwa mtumishi wako, ukisema, ‘Nitakujengea nyumba.’ Hivyo mtumishi wako amepata ujasiri kukuletea dua hii.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ee bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, umelifunua hili kwa mtumishi wako, ukisema, ‘Nitakujengea nyumba.’ Hivyo mtumishi wako amepata ujasiri kukuletea dua hii.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa wewe, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli umenifunulia mimi, mtumishi wako, ukisema, Nitakujengea nyumba; kwa hiyo mimi, mtumishi wako, nimepata ujasiri nikuombe ombi hili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana wewe, ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, umenifunulia mimi mtumishi wako, ukisema ‘Nitakujengea nyumba;’ ndio maana nina ujasiri kutoa ombi hili mbele yako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani wewe Bwana Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, umelifunua sikio la mtumishi wako, asikie ya kwamba: Mimi nitakujengea nyumba. Kwa hiyo mtumishi wako amejipa moyo wa kukuomba maombo haya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa wewe, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli umenifunulia mimi, mtumwa wako, ukisema, Nitakujengea nyumba; kwa hiyo mimi, mtumwa wako, nimeona vema moyoni mwangu nikuombe dua hii.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maana wewe, ee Yawe wa majeshi, Mungu wa Israeli, umenifunulia mimi mutumishi wako, ukisema: ‘Nitakujengea nyumba’; ndiyo maana nina uhodari wa kutoa ombi hili mbele yako.