2 Samuel 8:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya hayo, Daudi aliwapiga, akawashinda Wafilisti. Akauteka mji wa Metheg-ama kutoka utawala wa Wafilisti.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya muda, Daudi akawashinda Wafilisti na kuwatiisha, naye akatwaa Metheg-Amma kutoka mikononi mwa Wafilisti.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa baadaye, Daudi akawapiga Wafilisti, akawashinda; Daudi akautwaa Gathi na vijiji vyake mikononi mwa hao Wafilisti.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya hayo, Daudi aliwapiga, akawashinda Wafilisti. Akauteka mji wa Metheg-ama kutoka utawala wa Wafilisti.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ikawa baada ya jambo hili, Daudi akawashinda Wafilisti na kuwatiisha, akateka Metheg-Amma kutoka mikononi mwa Wafilisti.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya muda, Daudi akawashinda Wafilisti na kuwatiisha, naye akautwaa Metheg-Amma kutoka mikononi mwa Wafilisti.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa baadaye, Daudi akawapiga Wafilisti, akawashinda; Daudi akautwaa Gathi na vijiji vyake mikononi mwa hao Wafilisti.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya hayo, Daudi aliwapiga, akawashinda Wafilisti. Akauteka mji wa Metheg-ama kutoka utawala wa Wafilisti.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hayo yalipokwisha, Dawidi akawapiga Wafilisti, akawashinda; kisha Dawidi akaishika mwenyewe hatamu ya mji mkuu, isishikwe tena na Wafilisti.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa baadaye, Daudi akawapiga Wafilisti, akawashinda; Daudi akautwaa Gathi na vijiji vyake mikononi mwa hao Wafilisti.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyuma ya hayo, Daudi aliwashinda Wafilistini. Akawanyenyekeza na kunyanganya utawala wa Wafilistini.