2 Samuel 8:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
alimtuma mwanawe Yoramu kwa mfalme Daudi kumpelekea salamu na pongezi kwa sababu alikuwa amepigana na Hadadezeri na kumshinda. Maana Hadadezeri alipigana na Toi mara nyingi. Yoramu alimpelekea Daudi zawadi za vyombo vya fedha, dhahabu na shaba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
akamtuma mwanawe Yoramu kwa Mfalme Daudi kumsalimu na kumpongeza kwa ushindi wake katika vita dhidi ya Hadadezeri, kwa kuwa Hadadezeri alikuwa amepigana vita na Tou. Yoramu akamletea Daudi vyombo vya fedha, dhahabu na shaba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tou akamtuma kwa Daudi Hadoramu mwanawe kusalimia, na kumbarikia, kwa sababu amepigana na Hadadezeri, na kumpiga; kwa maana Hadadezeri alikuwa amepigana vita juu ya Tou. Na mkononi mwake akaleta vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu, na vyombo vya shaba;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
alimtuma mwanawe Yoramu kwa mfalme Daudi kumpelekea salamu na pongezi kwa sababu alikuwa amepigana na Hadadezeri na kumshinda. Maana Hadadezeri alipigana na Toi mara nyingi. Yoramu alimpelekea Daudi zawadi za vyombo vya fedha, dhahabu na shaba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
akamtuma Yoramu mwanawe kwa Mfalme Daudi kumsalimu na kumpongeza kwa ajili ya ushindi wake katika vita juu ya Hadadezeri, kwa maana Hadadezeri alikuwa amepigana vita na Tou. Yoramu akamletea Daudi vyombo vya fedha, dhahabu na shaba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
akamtuma mwanawe Yoramu kwa Mfalme Daudi kumsalimu na kumpongeza kwa ushindi wake katika vita dhidi ya Hadadezeri, kwa kuwa Hadadezeri alikuwa amepigana vita na Tou. Yoramu akamletea Daudi vyombo vya fedha, dhahabu na shaba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tou akamtuma Yoramu mwanawe kwa mfalme Daudi ili kumsalimia, na kumpongeza, na kumbariki, kwa sababu amepigana na Hadadezeri, na kumpiga; kwa maana Hadadezeri alikuwa amepigana vita juu ya Tou. Na mkononi mwake Yoramu akaleta vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu, na vyombo vya shaba;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
alimtuma mwanawe Yoramu kwa mfalme Daudi kumpelekea salamu na pongezi kwa sababu alikuwa amepigana na Hadadezeri na kumshinda. Maana Hadadezeri alipigana na Toi mara nyingi. Yoramu alimpelekea Daudi zawadi za vyombo vya fedha, dhahabu na shaba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Toi akamtuma mwanawe Yoramu kwake mfalme Dawidi kumpongeza na kumbariki, kwa kuwa amepigana na Hadadezeri na kumshinda, kwani Toi na Hadadezeri walikuwa wakipigana vita, naye akampelekea mkononi mwake vyombo vya fedha na vyombo vya dhahabu na vyombo vya shaba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tou akamtuma kwa Daudi Hadoramu mwanawe kusalimia, na kumbarikia, kwa sababu amepigana na Hadadezeri, na kumpiga; kwa maana Hadadezeri alikuwa amepigana vita juu ya Tou. Na mkononi mwake akaleta vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu, na vyombo vya shaba;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
alimutuma mwana wake Yoramu kwa mufalme Daudi kwa kumupelekea salamu na shukrani kwa sababu alikuwa amepigana na Hadadezeri na kumushinda. Maana Hadadezeri alipigana na Toi mara nyingi. Yoramu alimupelekea Daudi zawadi za vyombo vya feza, zahabu na shaba.