2 Samuel 8:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Daudi alijiongezea umaarufu wake. Alipokuwa anarudi baada ya kumshinda Hadadezeri, aliwaua Waedomu 18,000, katika Bonde la Chumvi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Naye Daudi akapata sifa baada ya kurudi kutoka kuwaua Waedomu elfu kumi na nane katika Bonde la Chumvi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Daudi akajipatia jina, aliporudi kutoka kuwapiga Waedomi katika Bonde la Chumvi, watu kumi na nane elfu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Daudi alijiongezea umaarufu wake. Alipokuwa anarudi baada ya kumshinda Hadadezeri, aliwaua Waedomu 18,000, katika Bonde la Chumvi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Naye Daudi akajulikana baada ya kurudi kutoka kuwaua Waedomu 18,000 katika Bonde la Chumvi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Naye Daudi akapata sifa baada ya kurudi kutoka kuwaua Waedomu 18,000 katika Bonde la Chumvi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Daudi akajipatia jina, alipokuwa akirudi, aliwaua Waedomi elfu kumi na nne katika bonde la chumvi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Daudi alijiongezea umaarufu wake. Alipokuwa anarudi baada ya kumshinda Hadadezeri, aliwaua Waedomu 18,000, katika Bonde la Chumvi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Dawidi aliporudi kwa kuwapiga Washami akajipatia jina kuu kwa kuua watu 18000 Bondeni kwa Chumvi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Daudi akajipatia jina, aliporudi kutoka kuwapiga Waedomi katika Bonde la Chumvi, watu kumi na nane elfu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Daudi alijiongezea sifa yake. Alipokuwa anarudi kisha kumushinda Hadadezeri, aliwaua Waedomu elfu kumi na nane, katika Bonde la Chumvi.