2 Samuel 8:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha aliwashinda Wamoabu. Aliwapanga katika mistari mateka hao, na kuwalaza chini. Aliamuru wale waliokuwa katika mistari miwili wauawe na wale wa mstari wa tatu waachwe hai. Hivyo, Wamoabu wakawa watumishi wake Daudi na wakawa wanamlipa kodi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Pia Daudi akawashinda Wamoabu. Akawafanya walale chini kwa mstari akawapima kwa urefu wa kamba. Kila alipopima urefu wa hiyo kamba mara mbili, hilo kundi waliuawa, na alipopima mara ya tatu aliwaacha hai. Kwa hiyo Wamoabu wakawa chini ya Daudi nao wakamletea ushuru.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akapiga Moabu, akawapima kwa kamba hali wamelazwa chini; akapima kamba mbili za kuuawa, na kamba moja nzima ya kuhifadhi hai. Wamoabi wakawa watumwa wa Daudi, wakaleta zawadi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha aliwashinda Wamoabu. Aliwapanga katika mistari mateka hao, na kuwalaza chini. Aliamuru wale waliokuwa katika mistari miwili wauawe na wale wa mstari wa tatu waachwe hai. Hivyo, Wamoabu wakawa watumishi wake Daudi na wakawa wanamlipa kodi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Pia Daudi akawashinda Wamoabu. Akawafanya walale chini kwa mstari akawapima kwa urefu wa kamba. Kila alipopima urefu wa hiyo kamba mara mbili hilo kundi waliuawa na alipopima mara ya tatu aliwaacha hai. Kwa hiyo Wamoabu wakawa chini ya Daudi nao wakamletea kodi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Pia Daudi akawashinda Wamoabu. Akawafanya walale chini kwa mstari akawapima kwa urefu wa kamba. Kila alipopima urefu wa hiyo kamba mara mbili hilo kundi waliuawa na alipopima mara ya tatu aliwaacha hai. Kwa hiyo Wamoabu wakawa chini ya Daudi nao wakamletea kodi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akapiga Moabu, akawapima kwa kamba wakiwa wamelazwa chini; akapima kamba mbili za kuuawa, na kamba moja nzima ya kuhifadhi hai. Wamoabi wakawa watumishi wa Daudi, wakaleta zawadi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha aliwashinda Wamoabu. Aliwapanga katika mistari mateka hao, na kuwalaza chini. Aliamuru wale waliokuwa katika mistari miwili wauawe na wale wa mstari wa tatu waachwe hai. Hivyo, Wamoabu wakawa watumishi wake Daudi na wakawa wanamlipa kodi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao Wamoabu akawapiga, akawapima kwa kamba akiwalaza chini, akapima hivyo: wa kamba mbili wakawa wa kuuawa, nao wote wa kamba moja wakawa wa kuachwa uzimani; nao Wamoabu wakawa watumishi wa Dawidi, wakamletea mahongo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akapiga Moabu, akawapima kwa kamba hali wamelazwa chini; akapima kamba mbili za kuuawa, na kamba moja nzima ya kuhifadhi hai. Wamoabi wakawa watumwa wa Daudi, wakaleta zawadi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha aliwashinda Wamoabu. Aliwapanga katika mistari mateka hao, na kuwalalisha chini. Aliamuru wale waliokuwa katika mistari miwili wauawe na wale wa mustari wa tatu waachwe wazima. Hivyo, Wamoabu wakakuwa watumishi wa Daudi na wakakuwa wanamulipa kodi.