2 Samuel 8:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Daudi aliteka wapandafarasi 1,700, na askari wa miguu 20,000. Kisha Daudi alikata mishipa ya miguu ya nyuma ya farasi wote wa magari, ila alibakiza farasi wa kutosheleza magari 100.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Daudi akateka magari yake ya vita elfu moja, waendesha hayo magari ya vita elfu saba, na askari wa miguu elfu ishirini. Daudi akawakata mishipa farasi wa magari ya vita, akabakiza farasi mia moja.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Daudi akampokonya wapanda farasi elfu na mia saba na askari waliokwenda kwa miguu ishirini elfu; Daudi akawakata mshipa farasi wote wa magari, ila farasi wa magari mia akawasaza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Daudi aliteka wapandafarasi 1,700, na askari wa miguu 20,000. Kisha Daudi alikata mishipa ya miguu ya nyuma ya farasi wote wa magari, ila alibakiza farasi wa kutosheleza magari 100.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Daudi akateka magari yake ya vita 1,000, askari wapanda farasi 7,000 na askari 20,000 watembeao kwa miguu. Daudi akawakata wale farasi wote wakokotao magari mishipa ya miguu, isipokuwa farasi 100 hakuwakata.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Daudi akateka magari yake ya vita 1,000, askari wapanda farasi 7,000 na askari 20,000 watembeao kwa miguu. Daudi akawakata wale farasi wote wakokotao magari mishipa ya miguu, isipokuwa farasi 100 hakuwakata.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Daudi akampokonya wapanda farasi elfu moja na mia saba na askari waliokwenda kwa miguu elfu ishirini; Daudi akawakata mshipa farasi wote wa magari, ila farasi wa magari mia moja akawabakiza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Daudi aliteka wapandafarasi 1,700, na askari wa miguu 20,000. Kisha Daudi alikata mishipa ya miguu ya nyuma ya farasi wote wa magari, ila alibakiza farasi wa kutosheleza magari 100.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Dawidi akateka kwake wapanda farasi 1700 na askari waliokwenda kwa miguu 20000, nao farasi wote wa kuvuta magari Dawidi akawakata mishipa, akajisazia farasi wa magari mia tu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Daudi akampokonya wapanda farasi elfu na mia saba na askari waliokwenda kwa miguu ishirini elfu; Daudi akawakata mshipa farasi wote wa magari, ila farasi wa magari mia akawasaza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Daudi aliteka waaskari wapanda-farasi elfu moja na mia saba, na waaskari wa miguu elfu makumi mbili. Kisha Daudi alikata mishipa ya miguu ya nyuma ya farasi wote wa magari ya vita, lakini aliacha farasi wa kutoshelea kwa magari mia moja.