2 Samuel 8:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Halafu Daudi aliweka kambi za kijeshi katika mji wa Waaramu wa Damasko. Basi, Waaramu wakawa watumishi wake na wakawa wanamlipa kodi. Mwenyezi-Mungu alimpa Daudi ushindi kokote alikokwenda.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Daudi akaweka askari walinzi katika ufalme wa Waaramu huko Dameski, nao Waaramu wakawa watumwa wake na kumlipa ushuru. Mwenyezi Mungu akampa Daudi ushindi kote alipoenda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Daudi akaweka ngome katika Shamu ya Dameski, na hao Washami wakawa watumwa wa Daudi, wakaleta zawadi. Naye Bwana akampa Daudi kushinda kila alikokwenda.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Halafu Daudi aliweka kambi za kijeshi katika mji wa Waaramu wa Damasko. Basi, Waaramu wakawa watumishi wake na wakawa wanamlipa kodi. Mwenyezi-Mungu alimpa Daudi ushindi kokote alikokwenda.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Daudi akaweka askari walinzi katika ufalme wa Waaramu huko Dameski, nao Waaramu wakawa chini yake na kumlipa kodi. BWANA akampa Daudi ushindi ko kote alikokwenda.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Daudi akaweka askari walinzi katika ufalme wa Waaramu huko Dameski, nao Waaramu wakawa watumwa wake na kumlipa ushuru. bwana akampa Daudi ushindi kote alipokwenda.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Daudi akaweka ngome katika Shamu ya Dameski, na hao Washami wakawa watumishi wa Daudi, wakaleta zawadi. Naye BWANA akampa Daudi kushinda kila alikokwenda.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Halafu Daudi aliweka kambi za kijeshi katika mji wa Waaramu wa Damasko. Basi, Waaramu wakawa watumishi wake na wakawa wanamlipa kodi. Mwenyezi-Mungu alimpa Daudi ushindi kokote alikokwenda.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Dawidi akaweka askari kwao Washami wa Damasko, hao Washami wakawa watumishi wa Dawidi, wakamletea mahongo, ndivyo, Bwana alivyompa Dawidi kushinda po pote, alipokwenda.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Daudi akaweka ngome katika Shamu ya Dameski, na hao Washami wakawa watumwa wa Daudi, wakaleta zawadi. Naye BWANA akampa Daudi kushinda kila alikokwenda.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Daudi aliweka kambi za waaskari katika muji wa Waaramu wa Damasiki. Basi, Waaramu wakakuwa watumishi wake na wakakuwa wanamulipa kodi. Yawe alimupa Daudi ushindi kokote alikokwenda.