2 Samuel 9:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme akamwuliza, “Je, hakuna mtu yeyote aliyesalia katika jamaa ya Shauli? Kama yuko, ningependa kumtendea wema wa Mungu.” Siba akamjibu, “Yuko mwana wa Yonathani, lakini yeye amelemaa miguu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme akamuuliza, “Je, hakuna yeyote ambaye amebaki wa nyumba ya Sauli ninayeweza kumwonesha wema wa Mungu?” Siba akamjibu mfalme, “Bado yupo mwana wa Yonathani; yeye ni kiwete kwenye miguu yote.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mfalme akasema, Je! Hakuna hata sasa mtu ye yote wa nyumba ya Sauli, nipate kumtendea mema ya Mungu? Siba akamwambia mfalme, Yonathani anaye mwana hata sasa, aliye na kilema cha mguu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme akamwuliza, “Je, hakuna mtu yeyote aliyesalia katika jamaa ya Shauli? Kama yuko, ningependa kumtendea wema wa Mungu.” Siba akamjibu, “Yuko mwana wa Yonathani, lakini yeye amelemaa miguu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme akauliza, “Je, hakuna ye yote ambaye amebaki wa nyumba ya Sauli ninayeweza kumwonyesha wema wa Mungu?” Siba akamjibu mfalme, “Bado yupo mwana wa Yonathani, yeye ni kiwete miguu yote.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme akauliza, “Je, hakuna yeyote ambaye amebaki wa nyumba ya Sauli ninayeweza kumwonyesha wema wa Mungu?” Siba akamjibu mfalme, “Bado yupo mwana wa Yonathani, yeye ni kiwete miguu yote.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mfalme akasema, Je! Hakuna hata sasa mtu yeyote wa nyumba ya Sauli, nipate kumtendea mema ya Mungu? Siba akamwambia mfalme, Yonathani anaye mwana hata sasa, aliye na kilema cha mguu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme akamwuliza, “Je, hakuna mtu yeyote aliyesalia katika jamaa ya Shauli? Kama yuko, ningependa kumtendea wema wa Mungu.” Siba akamjibu, “Yuko mwana wa Yonathani, lakini yeye amelemaa miguu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfalme akamwuliza: Yuko bado mtu wa mlango wa Sauli, nimgawie mema ya Mungu? Siba akamwambia mfalme: Yuko bado mwana wa Yonatani, naye amelemaa miguu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mfalme akasema, Je! Hakuna hata sasa mtu ye yote wa nyumba ya Sauli, nipate kumtendea mema ya Mungu? Siba akamwambia mfalme, Yonathani anaye mwana hata sasa, aliye na kilema cha mguu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme akamwuliza: “Hakuna hata mutu mumoja aliyebaki katika jamaa ya Saulo? Kama yuko, ningependa kumutendea wema wa Mungu.” Siba akamujibu: “Kuko mwana wa Yonatani. Yeye ni kilema.”