2 Thessalonians 1:10 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
wakati atakapokuja siku ile kupokea utukufu kutoka kwa watu wake na heshima kutoka kwa wote wanaoamini. Nyinyi pia mtakuwa miongoni mwao, kwani mmeuamini ule ujumbe tuliowaletea.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
siku hiyo atakapokuja kutukuzwa katika watakatifu wake na kustaajabiwa miongoni mwa wote walioamini. Ninyi pia mtakuwa miongoni mwa hawa kwa sababu mliamini ushuhuda wetu kwenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
yeye atakapokuja ili kutukuzwa katika watakatifu wake, na kustaajabiwa katika wote waliosadiki katika siku ile, (kwa sababu ushuhuda wetu ulisadikiwa kwenu).
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hii itatokea siku ambapo Bwana Yesu atakuja na kupokea heshima miongoni mwa watu wake watakatifu. Na wote wanaomwamini watamstaajabu. Na hii inawajumuisha ninyi kwa sababu mliamini yale tuliyowaambia.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
wakati atakapokuja Siku ile kupokea utukufu kutoka kwa watu wake na heshima kutoka kwa wote wanaoamini. Ninyi pia mtakuwa miongoni mwao, kwani mmeuamini ule ujumbe tuliowaletea.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
wakati atakapokuja siku ile kupokea utukufu kutoka kwa watu wake na heshima kutoka kwa wote wanaoamini. Nyinyi pia mtakuwa miongoni mwao, kwani mmeuamini ule ujumbe tuliowaletea.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
siku hiyo atakapokuja kutukuzwa katika watakatifu wake na kustaajabiwa miongoni mwa wote walioamini. Ninyi pia mtakuwa miongoni mwa hawa kwa sababu mliamini ushuhuda wetu kwenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
siku hiyo atakapokuja kutukuzwa katika watakatifu wake na kustaajabiwa miongoni mwa wote walioamini. Ninyi pia mtakuwa miongoni mwa hawa kwa sababu mliamini ushuhuda wetu kwenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
yeye atakapokuja ili kutukuzwa katika watakatifu wake, na kustaajabiwa katika wote waliosadiki katika siku ile, (kwa sababu ushuhuda wetu ulisadikiwa kwenu).
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
wakati atakapokuja siku ile kupokea utukufu kutoka kwa watu wake na heshima kutoka kwa wote wanaoamini. Nyinyi pia mtakuwa miongoni mwao, kwani mmeuamini ule ujumbe tuliowaletea.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivi vitakuwa siku ileile, atakapokuja kutukuzwa kati ya watakatifu wake na kustaajabiwa kati yao wote wamtegemeao; kwani mambo hayo, tuliyoyashuhudia, yalipata kwenu wenye kuyategemea.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
yeye atakapokuja ili kutukuzwa katika watakatifu wake, na kustaajabiwa katika wote waliosadiki katika siku ile, (kwa sababu ushuhuda wetu ulisadikiwa kwenu).
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
atakapokuja apate kutukuzwa na watu wake na kushangiliwa na wale wote wanaoamini. Ninyi vilevile mutakuwa pamoja nao kwa maana mumeamini habari tuliyowatangazia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
atakapokuja illi kutukuzwa katika watakatifu wake, na kuajabiwa katika wote waaminio (kwa sababu ushuhuda wetu ulisadikiwa kwenu), katika siku ile.