2 Thessalonians 1:11 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndiyo maana tunawaombeeni daima. Tunamwomba Mungu wetu awawezesheni kustahili maisha aliyowaitia muyaishi. Tunamwomba, kwa uwezo wake, atimize nia yenu ya kutenda mema na kukamilisha kazi yenu ya imani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa sababu hii, tunawaombea ninyi bila kukoma, ili Mungu wetu apate kuwahesabu kuwa mnastahili wito wake na kwamba kwa uwezo wake apate kutimiza kila kusudi lenu jema na kila tendo linaloongozwa na imani yenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa hiyo twawaombea ninyi sikuzote, ili Mungu wetu awahesabu kuwa mmekustahili kuitwa kwenu, akatimiza kila haja ya wema na kila kazi ya imani kwa nguvu;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hii ndiyo sababu daima tunawaombea. Tunamwomba Mungu wetu awasaidie kuishi katika njia njema aliyoitaka alipowachagua. Wema mlionao unawafanya mtake kufanya mema. Na imani mliyonayo inafanya mfanye kazi. Tunaomba kwamba kupitia nguvu zake Mungu atayakamilisha yote mema mliyokusudia kufanya pamoja na kazi zote zinazotokana na imani yenu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ndiyo maana tunawaombeeni daima. Tunamwomba Mungu wetu awawezeshe muyastahili maisha aliyowaitia myaishi. Tunamwomba, kwa uwezo wake, atimize nia yenu ya kutenda mema na kukamilisha kazi yenu ya imani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndiyo maana tunawaombeeni daima. Tunamwomba Mungu wetu awawezesheni kustahili maisha aliyowaitia muyaishi. Tunamwomba, kwa uwezo wake, atimize nia yenu ya kutenda mema na kukamilisha kazi yenu ya imani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa sababu hii, tunawaombea ninyi bila kukoma, ili kwamba Mungu apate kuwahesabu kuwa mnastahili wito wake na kwamba kwa uwezo wake apate kutimiza kila kusudi lenu jema na kila tendo linaloongozwa na imani yenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa sababu hii, tunawaombea ninyi bila kukoma, ili Mwenyezi Mungu apate kuwahesabu kuwa mnastahili wito wake na kwamba kwa uwezo wake apate kutimiza kila kusudi lenu jema na kila tendo linaloongozwa na imani yenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa hiyo tunawaombea ninyi siku zote, ili Mungu wetu awahesabu kuwa mmekustahili kuitwa kwenu, akatimiza kila haja ya wema na kila kazi ya imani kwa nguvu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndiyo maana tunawaombeeni daima. Tunamwomba Mungu wetu awawezesheni kustahili maisha aliyowaitia muyaishi. Tunamwomba, kwa uwezo wake, atimize nia yenu ya kutenda mema na kukamilisha kazi yenu ya imani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa ajili ya neno hili twawaombea ninyi siku zote, Mungu wetu awape kufanya mwenendo uupasao wito wenu, mpate nguvu za kuyatimiza mema yote yaliyowapendeza na za kufanya matendo yafanyikayo kwa kumtegemea.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa hiyo twawaombea ninyi sikuzote, ili Mungu wetu awahesabu kuwa mmekustahili kuitwa kwenu, akatimiza kila haja ya wema na kila kazi ya imani kwa nguvu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa sababu hii tunawaombea siku zote kusudi Mungu wetu awawezeshe kustahili kuishi kufuatana na mwito wake. Tunaomba kwamba kwa uwezo wake atimize nia zenu zote njema na kukamilisha kazi yenu ya imani.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa hiyo twawaombea ninyi siku zote, illi Mungu wetu awahesabu kuwa nimeustahili wito wenu, akatimize killa haja ya wema na killa kazi ya imani kwa nguvu: