2 Thessalonians 1:12 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa namna hiyo, jina la Bwana wetu Yesu litapata utukufu kutoka kwenu, nanyi mtapata utukufu kutoka kwake kwa neema ya Mungu wetu na ya Bwana Yesu Kristo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tunaomba hivi ili Jina la Bwana wetu Isa lipate kutukuzwa ndani yenu, nanyi ndani yake, kulingana na neema ya Mungu wetu na Bwana Isa Al-Masihi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
jina la Bwana wetu Yesu litukuzwe ndani yenu, nanyi ndani yake, kwa neema ya Mungu wetu na ya Bwana Yesu Kristo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha jina la Bwana wetu Yesu litaheshimiwa kwa sababu yenu, nanyi mtaheshimiwa kwa sababu yake, na mtaheshimiwa kwa sababu yake. Hii inaweza kutokea tu kwa neema ya Mungu wetu na Bwana Yesu Kristo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa namna hiyo, jina la Bwana wetu Yesu litapata utukufu kutoka kwenu, nanyi mtapata utukufu kutoka kwake kwa neema ya Mungu wetu na ya Bwana Yesu Kristo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa namna hiyo, jina la Bwana wetu Yesu litapata utukufu kutoka kwenu, nanyi mtapata utukufu kutoka kwake kwa neema ya Mungu wetu na ya Bwana Yesu Kristo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tunaomba hivi ili Jina la Bwana wetu Yesu lipate kutukuzwa ndani yenu, nanyi ndani yake, kulingana na neema ya Mungu wetu na Bwana Yesu Kristo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tunaomba hivi ili Jina la Bwana wetu Isa lipate kutukuzwa ndani yenu, nanyi ndani yake, kulingana na neema ya Mungu wetu na Bwana Isa Al-Masihi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
jina la Bwana wetu Yesu litukuzwe ndani yenu, nanyi ndani yake, kwa neema ya Mungu wetu na ya Bwana Yesu Kristo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa namna hiyo, jina la Bwana wetu Yesu litapata utukufu kutoka kwenu, nanyi mtapata utukufu kutoka kwake kwa neema ya Mungu wetu na ya Bwana Yesu Kristo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo ndivyo, Jina la Bwana wetu Yesu litakavyotukuzwa mwenu, nanyi mtatukuzwa mwake, yatakapotimia yale, Mungu wetu na Bwana Yesu Kristo aliyowagawia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
jina la Bwana wetu Yesu litukuzwe ndani yenu, nanyi ndani yake, kwa neema ya Mungu wetu na ya Bwana Yesu Kristo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hivi mutatukuza jina la Bwana wetu Yesu, nanyi mutatukuzwa naye kwa neema ya Mungu wetu na ya Bwana Yesu Kristo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
jina la Bwana wetu Yesu litukuzwe kwenu, na ninyi ndani yake, kwa neema ya Mungu wetu na ya Bwana Yesu Kristo.