2 Thessalonians 1:3 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndugu, tunapaswa kumshukuru Mungu daima kwa ajili yenu. Inafaa kwetu kufanya hivyo kwani imani yenu inakua sana na kupendana kwenu kunaongezeka sana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndugu, inatupasa kumshukuru Mungu kwa ajili yenu siku zote, na inastahili hivyo kwa sababu imani yenu inazidi kukua sana, nao upendo wa kila mmoja wenu kwa mwenzake unazidi kuongezeka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndugu, imetupasa kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, kama ilivyo wajibu, kwa kuwa imani yenu inazidi sana, na upendo wa kila mtu kwenu kwa mwenzake umekuwa mwingi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kaka na dada zetu, tunamshukuru Mungu kwa ajili yenu. Na hivyo ndivyo tunavyopaswa kufanya, kwani mnatupa sababu ya kushukuru na imani yenu inakua zaidi na zaidi. Pamoja na hilo upendo ambao kila mmoja wenu anao kwa mwenzake nao unakua.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ndugu, tunapaswa kushukuru Mungu daima kwa ajili yenu. Inafaa kwetu kufanya hivyo kwani imani yenu inakua sana na kupendana kwenu kunaongezeka sana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndugu, tunapaswa kumshukuru Mungu daima kwa ajili yenu. Inafaa kwetu kufanya hivyo kwani imani yenu inakua sana na kupendana kwenu kunaongezeka sana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndugu, imetubidi kumshukuru Mungu kwa ajili yenu siku zote, kama ulivyo wajibu wetu, kwa sababu imani yenu inakua zaidi na zaidi na upendo wa kila mmoja wenu alio nao kwa mwenzake unazidi kuongezeka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndugu, imetubidi kumshukuru Mungu kwa ajili yenu siku zote, kama ulivyo wajibu wetu, kwa sababu imani yenu inakua zaidi na zaidi na upendo wa kila mmoja wenu alio nao kwa mwenzake unazidi kuongezeka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndugu, imetupasa kumshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, kama ilivyo wajibu, kwa kuwa imani yenu inazidi sana, na upendo wa kila mtu kwenu kwa mwenzake umekuwa mwingi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndugu, tunapaswa kumshukuru Mungu daima kwa ajili yenu. Inafaa kwetu kufanya hivyo kwani imani yenu inakua sana na kupendana kwenu kunaongezeka sana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Sharti tumshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, ndugu; hii inatupasa, kwa sababu nguvu zenu za kumtegemea Mungu zinaongezeka sana, nao upendano unakua, maana ninyi nyote kila mmoja wenu humpenda mwenzake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndugu, imetupasa kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, kama ilivyo wajibu, kwa kuwa imani yenu inazidi sana, na upendo wa kila mtu kwenu kwa mwenzake umekuwa mwingi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wandugu, tunapaswa kumushukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu. Inatufaa kufanya vile kwa maana imani yenu inaongezeka, nao upendo wenu ninyi kwa ninyi unazidi kuongezeka.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Imetupasa kumshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, ndugu, kama ilivyo wajib, kwa kuwa imani yenu inazidi sana, na upendo wa killa mtu kwenu kwa wenzake umekuwa mwingi.