2 Thessalonians 1:4 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndio maana sisi tunajivunia nyinyi katika makanisa ya Mungu. Tunaona fahari juu ya jinsi mnavyoendelea kuamini na kustahimili katika udhalimu wote na mateso mnayopata.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndiyo sababu miongoni mwa makundi ya waumini ya Mungu, tunajivunia saburi yenu na imani mliyo nayo katika mateso yote na dhiki mnazostahimili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata na sisi wenyewe twaona fahari juu yenu katika makanisa ya Mungu kwa ajili ya saburi yenu, na imani mliyo nayo katika adha zenu zote na dhiki mnazostahimili.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo tunayaeleza makanisa mengine ya Mungu namna tunavyojivuna kuhusu ninyi. Tunawaeleza jinsi mlivyoendelea kwa subira kuwa imara na waaminifu, ingawa mnateswa na kusumbuliwa na matatizo mengi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ndio maana sisi tunajivunia ninyi katika makanisa ya Mungu. Tunaona fahari juu ya jinsi mnavyoendelea kuamini na kustahimili katika udhalimu wote na mateso mnayopata.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndio maana sisi tunajivunia nyinyi katika makanisa ya Mungu. Tunaona fahari juu ya jinsi mnavyoendelea kuamini na kustahimili katika udhalimu wote na mateso mnayopata.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndiyo sababu miongoni mwa makanisa ya Mungu, tunajivuna kuhusu saburi yenu na imani mliyo nayo katika mateso yote na dhiki mnazostahimili.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndiyo sababu miongoni mwa makundi ya waumini ya Mungu, tunajivuna kuhusu saburi yenu na imani mliyo nayo katika mateso yote na dhiki mnazostahimili.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata na sisi wenyewe tunaona fahari juu yenu katika makanisa ya Mungu kwa ajili ya subira yenu, na imani mliyo nayo katika adha zenu zote na dhiki mnazostahimili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndio maana sisi tunajivunia nyinyi katika makanisa ya Mungu. Tunaona fahari juu ya jinsi mnavyoendelea kuamini na kustahimili katika udhalimu wote na mateso mnayopata.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo hata sisi wenyewe twajivuna kwa ajili yenu katika wateule wa Mungu, kwamba mwavumilia, tena mwamtegemea Bwana katika mafukuzo na maumivu yenu yote, mnayojitwika.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata na sisi wenyewe twaona fahari juu yenu katika makanisa ya Mungu kwa ajili ya saburi yenu, na imani mliyo nayo katika adha zenu zote na dhiki mnazostahimili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kufuatana na ile, sisi tunajivuna kwa ajili yenu katika makanisa ya Mungu kwa sababu ya uvumilivu wenu na imani munayokuwa nayo katika mateso na taabu munazopata.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta sisi wenyewe twajisifu katika makanisa ya Mungu kwa ajili ya uvumilivu wenu, na imani mliyo nayo katika adha zenu zote na mateso mnayoyavumilia;