2 Thessalonians 1:5 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hayo yote yanathibitisha kwamba hukumu ya Mungu ni ya haki, na matokeo yake, nyinyi mtastahili ufalme wake ambao kwa ajili yake mnateseka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Haya yote ni uthibitisho kwamba hukumu ya Mungu ni ya haki, na kwa sababu hiyo ninyi mtahesabiwa kwamba mnastahili kuwa wa ufalme wa Mungu, mnaoteswa kwa ajili yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndiyo ishara hasa ya hukumu iliyo haki ya Mungu, ili mhesabiwe kuwa mwastahili kuuingia ufalme wa Mungu, ambao kwa ajili yake mnateswa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Huu ni uthibitisho kwamba Mungu ni wa haki katika hukumu zake. Hutaka kuwastahilisha katika ufalme wake. Kuteswa kwenu ni kwa ajili ya ufalme huo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hayo yote yanathibitisha kwamba hukumu ya Mungu ni ya haki, na matokeo yake ninyi mtastahili Utawala wake ambao kwa ajili yake mnateseka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hayo yote yanathibitisha kwamba hukumu ya Mungu ni ya haki, na matokeo yake, nyinyi mtastahili ufalme wake ambao kwa ajili yake mnateseka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Haya yote ni uthibitisho kwamba hukumu ya Mungu ni ya haki na kwa sababu hiyo ninyi mtahesabiwa kwamba mnastahili Ufalme wa Mungu, ambao ninyi mnateswa kwa ajili yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Haya yote ni uthibitisho kwamba hukumu ya Mungu ni ya haki, na kwa sababu hiyo ninyi mtahesabiwa kwamba mnastahili kuwa wa Ufalme wa Mwenyezi Mungu, mnaoteswa kwa ajili wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndiyo ishara hasa ya hukumu iliyo haki ya Mungu, ili mhesabiwe kuwa mwastahili kuuingia ufalme wa Mungu, ambao kwa ajili yake mnateswa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hayo yote yanathibitisha kwamba hukumu ya Mungu ni ya haki, na matokeo yake, nyinyi mtastahili ufalme wake ambao kwa ajili yake mnateseka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Humu ndimo, hukumu yake Mungu itakamoonekana kuwa ya kuongoka: ninyi mtaambiwa: Ufalme wa Mungu umewapasa kwa hivyo, mnavyoteswa kwa ajili yake huo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndiyo ishara hasa ya hukumu iliyo haki ya Mungu, ili mhesabiwe kuwa mwastahili kuuingia ufalme wa Mungu, ambao kwa ajili yake mnateswa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hayo yote yanahakikisha kwamba hukumu ya Mungu ni ya haki na matokeo yake ni kwamba ninyi munastahili kuingia katika Ufalme wake ambao kwa ajili yake ninyi munateseka.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
ndio ishara ya hukumu ya haki ya Mungu illi mstabilishwe kuuingia ufalme wa Mungu, ambao kwa ajili yake mnateswa;