2 Thessalonians 2:13 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tunapaswa kumshukuru Mungu daima kwa ajili yenu nyinyi ndugu, nyinyi mnaopendwa na Bwana, kwa maana Mungu amewateua tangu mwanzo mpate kuokolewa kwa nguvu ya Roho, mfanywe watu wake watakatifu kwa imani yenu katika ukweli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini inatupasa kumshukuru Mungu daima kwa ajili yenu, ndugu mpendwao na Bwana Isa, kwa sababu Mungu aliwachagua ninyi tangu mwanzo ili mwokolewe kwa kutakaswa na Roho wa Mungu kwa kuiamini kweli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, ndugu mliopendwa na Bwana, kwa kuwa Mungu amewachagua tangu mwanzo mpate wokovu, katika kutakaswa na Roho, na kuiamini kweli;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndugu zangu, ninyi ni watu mnaopendwa na Bwana. Na imetupasa tumshukuru Mungu daima kwa sababu yenu. Hayo ndiyo tunayotakiwa kuyatenda, kwa sababu Mungu aliwaita kuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuokolewa. Mmeokolewa na Roho aliyewafanya muwe watu wa Mungu walio watakatifu kupitia kuiamini kweli.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Tunapaswa kumshukuru Mungu daima kwa ajili yenu ninyi ndugu, ninyi mnaopendwa na Bwana, kwa maana Mungu amewateua tangu mwanzo mpate kuokolewa kwa nguvu ya Roho mfanywe watu wake watakatifu kwa imani yenu katika ukweli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tunapaswa kumshukuru Mungu daima kwa ajili yenu nyinyi ndugu, nyinyi mnaopendwa na Bwana, kwa maana Mungu amewateua tangu mwanzo mpate kuokolewa kwa nguvu ya Roho, mfanywe watu wake watakatifu kwa imani yenu katika ukweli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu daima kwa ajili yenu, ndugu mpendwao na Bwana, kwa sababu Mungu aliwachagua ninyi tangu mwanzo ili mwokolewe kwa kutakaswa na Roho kwa kuiamini kweli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mwenyezi Mungu daima kwa ajili yenu, ndugu mpendwao na Bwana Isa, kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwachagua ninyi tangu mwanzo ili mwokolewe kwa kutakaswa na Roho wa Mwenyezi Mungu kwa kuiamini kweli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, ndugu mliopendwa na Bwana, kwa kuwa Mungu amewachagua tangu mwanzo mpate wokovu, katika kutakaswa na Roho, na kuiamini kweli;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tunapaswa kumshukuru Mungu daima kwa ajili yenu nyinyi ndugu, nyinyi mnaopendwa na Bwana, kwa maana Mungu amewateua tangu mwanzo mpate kuokolewa kwa nguvu ya Roho, mfanywe watu wake watakatifu kwa imani yenu katika ukweli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndugu, sisi imetupasa kumshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu mliopendwa na Bwana, maana Mungu aliwachagua ninyi tangu mwanzo, mpate wokovu mkitakaswa roho, mkayategemea yaliyo ya kweli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, ndugu mliopendwa na Bwana, kwa kuwa Mungu amewachagua tangu mwanzo mpate wokovu, katika kutakaswa na Roho, na kuiamini kweli;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini sisi tunapaswa kumushukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu ninyi wandugu wapendwa wa Bwana. Kwa maana Mungu amewachagua ninyi wa kwanza kuwa watu wake kusudi mupate kuokolewa kwa kutakaswa na Roho Mutakatifu na kwa kuamini maneno ya ukweli.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, ndugu, mliopendwa na Bwana, kwa kuwa Mungu amewachagua tangu mwanzo mpate wokofu, katika kutakaswa kwa Roho na kuiamini kweli,