2 Thessalonians 2:6 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini kuna kitu kinachomzuia sasa, nanyi mwakijua kitu hicho. Basi, huyo Mwovu ataonekana wakati wake ufaao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nanyi sasa mnajua kinachomzuia, ili apate kudhihirishwa wakati wake utakapowadia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na mnafahamu kinachomzuia Mtu wa Uovu. Huyo hataruhusiwa kuonekana mpaka wakati sahihi utakapofika.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini kuna kitu kinachomzuia sasa, nanyi mwakijua kitu hicho. Basi, huyo Mwovu ataonekana wakati wake ufaao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini kuna kitu kinachomzuia sasa, nanyi mwakijua kitu hicho. Basi, huyo Mwovu ataonekana wakati wake ufaao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nanyi sasa mnajua kinachomzuia, ili kwamba apate kudhihirishwa wakati wake utakapowadia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nanyi sasa mnajua kinachomzuia, ili apate kudhihirishwa wakati wake utakapowadia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na sasa lizuialo mnalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini kuna kitu kinachomzuia sasa, nanyi mwakijua kitu hicho. Basi, huyo Mwovu ataonekana wakati wake ufaao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nacho kinachomzuia sasa mwakijua; lakini siku yake itakapotimia, atatokea waziwazi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini munajua kitu kinachozuiza mambo haya kutokea sasa. Kwa hivi yule Mwovu atatokea kwa wakati wake uliopangwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na sasa lizuialo mwalijua, apate kufunuliwa huyu wakati wake. Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi;