2 Thessalonians 2:7 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hata hivyo, Mwovu huyo aliyefichika anafanya kazi sasa, lakini hataonekana mpaka yule anayemzuia aondolewe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Maana ile nguvu ya siri ya uasi tayari inatenda kazi, lakini yule anayeizuia ataendelea kufanya hivyo hadi atakapoondolewa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tayari nguvu ya uovu inatenda kazi ulimwenguni sasa. Lakini yupo mmoja anayeizuia nguvu hiyo. Na ataendelea kuizuia mpaka atakapoondolewa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hata hivyo, Mwovu huyo aliyefichika anafanya kazi sasa, lakini hataonekana mpaka yule anayemzuia aondolewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hata hivyo, Mwovu huyo aliyefichika anafanya kazi sasa, lakini hataonekana mpaka yule anayemzuia aondolewe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Maana ile nguvu ya siri ya uasi tayari inatenda kazi, lakini yule anayeizuia ataendelea kufanya hivyo mpaka atakapoondolewa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Maana ile nguvu ya siri ya uasi tayari inatenda kazi, lakini yule anayeizuia ataendelea kufanya hivyo mpaka atakapoondolewa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inafanya kazi; lakini yuko azuiaye sasa, hadi atakapoondolewa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hata hivyo, Mwovu huyo aliyefichika anafanya kazi sasa, lakini hataonekana mpaka yule anayemzuia aondolewe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani ule upotovu uliokuwa umefichwa umekwisha anza kutenda nguvu, kisaacho ni hiki: yule mwenye kuuzuia mpaka sasa sharti aondolewe, atoke hapo kati.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hata hivi yule Mwovu anatenda kazi zake kwa siri; lakini yule anayezuiza ataendelea hata atakapoondoshwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
lakini yuko azuiae sasa, hatta atakapoondolewa.