2 Thessalonians 2:8 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo ndipo Mwovu atakapotokea; lakini Bwana Yesu anapokuja atamuua kwa pumzi ya kinywa chake na kumwangamiza kwa mngao wa kuja kwake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hapo ndipo yule mwasi atafunuliwa, ambaye Bwana Isa atamteketeza kwa pumzi ya kinywa chake na kumwangamiza kabisa kwa utukufu wa kuja kwake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha huyo Mtu wa Uovu atatokea. Lakini Bwana Yesu atamuua kwa pumzi inayotoka katika kinywa chake. Bwana atakuja katika namna ambayo kila mtu atamwona, na huo utakuwa mwisho wa Mtu wa Uovu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hapo ndipo Mwovu atakapotokea; lakini Bwana Yesu anapokuja atamuua kwa pumzi ya kinywa chake na kumwangamiza kwa mng'ao wa kuja kwake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo ndipo Mwovu atakapotokea; lakini Bwana Yesu anapokuja atamuua kwa pumzi ya kinywa chake na kumwangamiza kwa mng'ao wa kuja kwake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hapo ndipo yule mwasi atafunuliwa, ambaye Bwana Yesu atamteketeza kwa pumzi ya kinywa chake na kumwangamiza kabisa kwa utukufu wa kuja kwake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hapo ndipo yule mwasi atafunuliwa, ambaye Bwana Isa atamteketeza kwa pumzi ya kinywa chake na kumwangamiza kabisa kwa utukufu wa kuja kwake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hapo ndipo atakapofunuliwa yule mwasi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa dhihirisho la kuja kwake;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo ndipo Mwovu atakapotokea; lakini Bwana Yesu anapokuja atamuua kwa pumzi ya kinywa chake na kumwangamiza kwa mngao wa kuja kwake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha ndipo, yule mpotovu atakapofunuliwa. Naye Bwana Yesu atamwua akimpuzia tu kwa kinywa chake, atenguke kwa mwangaza wa kuja kwake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu, yule Mwovu atatokea, lakini Bwana Yesu atakapotokea atamwua kwa pumzi ya kinywa chake na kumwangamiza kwa nguvu za kumetameta kwake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambae Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa mafunuo ya kuwako kwake;