2 Thessalonians 2:9 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huyo Mwovu atakuja na nguvu za Shetani na kufanya kila namna ya miujiza na maajabu ya uongo,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kuja kwa yule mwasi kutalingana na vile Shetani hufanya kazi. Atatumia nguvu za aina mbalimbali katika miujiza, na ishara na ajabu za uongo,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kuja kwa Mtu wa Uovu itakuwa kazi ya Shetani. Atakuja na nguvu kuu, na atafanya aina zote za miujiza ya uongo, ishara, na maajabu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Huyo Mwovu atakuja na nguvu za Shetani na kufanya kila namna ya miujiza na maajabu ya uongo,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huyo Mwovu atakuja na nguvu za Shetani na kufanya kila namna ya miujiza na maajabu ya uongo,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kuja kwa yule mwasi kutaonekana kana kwamba ni kutenda kazi kwake Shetani ambaye hutumia nguvu zote, ishara, maajabu ya uongo
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kuja kwa yule mwasi kutaonekana kana kwamba ni kutenda kazi kwake Shetani ambaye hutumia nguvu zote, ishara, maajabu ya uongo,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kuja kwa yule mwasi ni kazi ya Shetani, atumiaye uwezo wote, ishara na ajabu za uongo;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huyo Mwovu atakuja na nguvu za Shetani na kufanya kila namna ya miujiza na maajabu ya uongo,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini yule mpotovu uwezo wa kuja kwake ni ule wa Satani, ukamfanyisha ya nguvu yo yote na vielekezo na vioja vya uwongo,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mwovu atakuja na uwezo wa Shetani na kufanya miujiza ya kila namna, vitambulisho na maajabu ya uongo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
ambae kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kazi kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za nwongo,