2 Thessalonians 3:1 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hatimaye, ndugu, tuombeeni ili ujumbe wa Bwana uzidi kuenea upesi na kupokelewa kwa heshima kama vile ulivyo kati yenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hatimaye, ndugu, tuombeeni ili Neno la Bwana Isa lipate kuenea kwa haraka na kuheshimiwa kila mahali, kama vile ilivyokuwa kwenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hatimaye, ndugu, tuombeeni, neno la Bwana liendelee, na kutukuzwa vile vile kama ilivyo kwenu;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na sasa, ndugu zangu, mtuombee. Ombeni kwamba mafundisho ya Bwana yaendelee kuenea haraka na kwamba watu watayaheshimu, kama ilivyotokea kwenu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hatimaye, ndugu, tuombeeni ili ujumbe wa Bwana uzidi kuenea upesi na kupokelewa kwa heshima kama vile ulivyo kati yenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hatimaye, ndugu, tuombeeni ili ujumbe wa Bwana uzidi kuenea upesi na kupokelewa kwa heshima kama vile ulivyo kati yenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hatimaye, ndugu, tuombeeni ili kwamba Neno la Bwana lipate kuenea kwa haraka na kuheshimiwa kila mahali, kama vile ilivyokuwa kwa upande wenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hatimaye, ndugu, tuombeeni ili Neno la Bwana Isa lipate kuenea kwa haraka na kuheshimiwa kila mahali, kama vile ilivyokuwa kwenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hatimaye, ndugu, tuombeeni, neno la Bwana liendelee, na kutukuzwa kote kama ilivyo kwenu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hatimaye, ndugu, tuombeeni ili ujumbe wa Bwana uzidi kuenea upesi na kupokelewa kwa heshima kama vile ulivyo kati yenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha, ndugu, mtuombee sisi kwa Mungu, Neno la Bwana liendelee na kutukuzwa vivyo hivyo kama kwenu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hatimaye, ndugu, tuombeeni, neno la Bwana liendelee, na kutukuzwa vile vile kama ilivyo kwenu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa mwisho wandugu, mutuombee, kusudi neno la Bwana lisambae upesi na kutukuzwa, kama vile inavyokuwa kwenu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
ILIYOBAKI, ndugu, tuombeeni, neno la Bwana liendelee, likatunzwe vilevile kama ilivyo kwenu;