2 Thessalonians 3:11 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tunasema mambo hayo kwa sababu tumesikia kwamba wako baadhi yenu ambao ni wavivu na ambao hawafanyi chochote, isipokuwa tu kujiingiza katika mambo ya watu wengine.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa tunasikia kwamba baadhi ya watu miongoni mwenu ni wavivu. Hawafanyi kazi, bali hujishughulisha na mambo ya wengine.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana twasikia kwamba wako watu kwenu waendao bila utaratibu, hawana shughuli zao wenyewe, lakini wanajishughulisha na mambo ya wengine.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tunasikia kwamba watu wengine katika kundi lenu wanakataa kufanya kazi. Hawashughuliki kufanya kazi badala yake wanashughulika kwa kuyafuatilia maisha ya wengine.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Tunasema mambo hayo kwa sababu tumesikia kwamba wako baadhi yenu ambao ni wavivu na ambao hawafanyi chochote, isipokuwa tu kujiingiza katika mambo ya watu wengine.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tunasema mambo hayo kwa sababu tumesikia kwamba wako baadhi yenu ambao ni wavivu na ambao hawafanyi chochote, isipokuwa tu kujiingiza katika mambo ya watu wengine.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa tunasikia kwamba baadhi ya watu miongoni mwenu ni wavivu. Hawafanyi kazi bali hujishughulisha na mambo ya wengine.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa tunasikia kwamba baadhi ya watu miongoni mwenu ni wavivu. Hawafanyi kazi bali hujishughulisha na mambo ya wengine.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana tunasikia kwamba wako watu kwenu waendao bila utaratibu, hawana shughuli zao wenyewe, lakini wanajishughulisha na mambo ya wengine.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tunasema mambo hayo kwa sababu tumesikia kwamba wako baadhi yenu ambao ni wavivu na ambao hawafanyi chochote, isipokuwa tu kujiingiza katika mambo ya watu wengine.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani twasikia: Kwenu wako wanaoendelea na kufuata mambo yaliyo ya ovyoovyo tu, hawafanyi kazi, ila hufanya mapuzi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana twasikia kwamba wako watu kwenu waendao bila utaratibu, hawana shughuli zao wenyewe, lakini wanajishughulisha na mambo ya wengine.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tunasema hivi kwa sababu tumepata habari kwamba wamoja kati yenu ni wavivu; hawatumiki, isipokuwa tu kujiingiza katika maneno ya wengine.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana twasikia kwamba wako watu kwenu waendao bila utaratibu, hawʼana shughuli yao wenyewe, bali wanajishughulisha na mambo ya wengine.