2 Thessalonians 3:17 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa mkono wangu mwenyewe naandika hivi: Salamu kutoka kwa Paulo! Hivi ndivyo ninavyotia sahihi kila barua; ndivyo ninavyoandika.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mimi, Paulo, ninaandika salamu hizi kwa mkono wangu mwenyewe. Hii ndio alama ya utambulisho katika barua zangu zote. Hivi ndivyo niandikavyo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Salamu zangu mimi Paulo, kwa mkono wangu mwenyewe. Hii ndiyo alama katika kila waraka, ndio mwandiko wangu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hizi ni salamu zangu kwa mwandiko wangu: PAULO. Ninafanya hivi katika barua zangu zote kuonesha zinatoka kwangu. Hivi ndivyo ninavyoandika.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa mkono wangu mwenyewe naandika hivi: Salamu kutoka kwa Paulo! Hivi ndivyo ninavyotia sahihi kila barua; ndivyo ninavyoandika.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa mkono wangu mwenyewe naandika hivi: Salamu kutoka kwa Paulo! Hivi ndivyo ninavyotia sahihi kila barua; ndivyo ninavyoandika.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mimi, Paulo, ninaandika salamu hizi kwa mkono wangu mwenyewe. Hii ndio alama ya utambulisho katika barua zangu zote. Hivi ndivyo niandikavyo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mimi, Paulo, ninaandika salamu hizi kwa mkono wangu mwenyewe. Hii ndio alama ya utambulisho katika barua zangu zote. Hivi ndivyo niandikavyo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Salamu zangu mimi Paulo, kwa mkono wangu mwenyewe. Hii ndiyo alama katika kila barua yangu, ndio mwandiko wangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa mkono wangu mwenyewe naandika hivi: Salamu kutoka kwa Paulo! Hivi ndivyo ninavyotia sahihi kila barua; ndivyo ninavyoandika.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Salamu hii naiandika kwa mkono wangu mimi Paulo; huu ndio mwandiko wangu katika barua zote. Hivi ndivyo, ninavyoandika.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Salamu zangu mimi Paulo, kwa mkono wangu mwenyewe. Hii ndiyo alama katika kila waraka, ndio mwandiko wangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hii ni salamu ninayoiandika kwa mukono wangu mimi Paulo mwenyewe. Hii ndiyo sahihi yangu katika kila barua yangu, na mwandiko wangu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Salamu zangu mimi Paolo, kwa mkono wangu mwenyewe. Hii ndiyo alama katika killa waraka, ndivyo niandikavyo.