2 Thessalonians 3:6 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndugu, tunawaamuru kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, mjiepushe na ndugu wote walio wavivu na ambao hawafuati maagizo tuliyowapa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndugu, tunawaagiza katika Jina la Bwana Isa Al-Masihi, jitengeni na kila ndugu ambaye ni mvivu na ambaye haishi kufuatana na maagizo tuliyowapa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndugu, twawaagiza katika jina la Bwana Yesu Kristo, jitengeni nafsi zenu na kila ndugu aendaye bila utaratibu, wala si kwa kufuata mapokeo mliyoyapokea kwetu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa mamlaka ya Bwana wetu Yesu Kristo tunawaambia kukaa mbali na mwamini yeyote anayekataa kufanya kazi. Watu kama hao wanaokataa kufanya kazi hawafuati mafundisho tuliyowapa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ndugu, tunawaamuru kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, mjiepushe na ndugu wote walio wavivu na ambao hawafuati maagizo tuliyowapa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndugu, tunawaamuru kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, mjiepushe na ndugu wote walio wavivu na ambao hawafuati maagizo tuliyowapa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndugu, tunawaagiza katika Jina la Bwana Yesu Kristo, jitengeni na kila ndugu ambaye ni mvivu na ambaye haishi kufuatana na maagizo tuliyowapa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndugu, tunawaagiza katika Jina la Bwana Isa Al-Masihi, jitengeni na kila ndugu ambaye ni mvivu na ambaye haishi kufuatana na maagizo tuliyowapa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndugu, tunawaagiza katika jina la Bwana Yesu Kristo, jitengeni nafsi zenu na kila ndugu aendaye bila utaratibu, wala si kwa kufuata mapokeo mliyoyapokea kwetu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndugu, tunawaamuru kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, mjiepushe na ndugu wote walio wavivu na ambao hawafuati maagizo tuliyowapa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Ndugu, tunawaagiza ninyi, kwa nguvu ya Jina la Bwana Yesu Kristo, mtengane na kila ndugu anayeendelea na kufuata mambo yaliyo ya ovyoovyo tu, asiufuate ufundisho, mlioupata kwetu sisi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndugu, twawaagiza katika jina la Bwana Yesu Kristo, jitengeni nafsi zenu na kila ndugu aendaye bila utaratibu, wala si kwa kufuata mapokeo mliyoyapokea kwetu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wandugu, tunawaagiza katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo kwamba mujitenge na wandugu wote wanaokuwa wavivu na wasiofuata mafundisho tuliyowapa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Twawaagizeni, ndugu, katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, jitengeni nafsi zenu na killa ndugu aendae bila utaratibu, wala si kwa kufuata mapokeo mliyoyapokea kwetu.