2 Thessalonians 3:9 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tulifanya hivyo si kwa kuwa hatuna haki ya kutaka msaada wenu, ila kwa sababu tunataka kuwapeni mfano.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tulifanya hivi, si kwa sababu hatukuwa na haki ya kupata msaada kama huo, bali ndio sisi wenyewe tuwe mfano wenu wa kufuata.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Si kwamba hatuna amri, lakini makusudi tufanye nafsi zetu kuwa kielelezo kwenu, mtufuate.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Tulikuwa na haki ya kuomba mtusaidie. Lakini tulifanya kazi ili tuwe mfano wa kuigwa nanyi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Tulifanya hivyo si kwa kuwa hatuna haki ya kutaka msaada wenu, ila kwa sababu tunataka kuwapeni mfano.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tulifanya hivyo si kwa kuwa hatuna haki ya kutaka msaada wenu, ila kwa sababu tunataka kuwapeni mfano.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tulifanya hivi, si kwa sababu hatukuwa na haki ya kupata msaada kama huo, lakini ili kusudi tujifanye sisi wenyewe kuwa kielelezo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tulifanya hivi, si kwa sababu hatukuwa na haki ya kupata msaada kama huo, bali ndio sisi wenyewe tuwe kielelezo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Si kwamba hatuna haki hiyo, ila kwa makusudi ya kuwapa mfano wa kuiga, mtufuate.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tulifanya hivyo si kwa kuwa hatuna haki ya kutaka msaada wenu, ila kwa sababu tunataka kuwapeni mfano.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hatukuvifanya hivyo kwamba: Hatu wakuu, ila tulitaka kuwapa ninyi vielezo, mpate kutuiga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Si kwamba hatuna amri, lakini makusudi tufanye nafsi zetu kuwa kielelezo kwenu, mtufuate.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tulifanya vile si kwa sababu hatukukuwa na haki ya kupokea musaada wenu, lakini kwa sababu tulitaka sisi wenyewe kuwa kwenu mufano wa kuiga.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
si kwamba hatuna uwezo, bali tufanye nafsi zetu kuwa mfano kwenu, mtufuate.