2 Timothy 1:10 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
lakini imefunuliwa kwetu sasa kwa kuja kwake Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Yeye amekomesha nguvu za kifo, na kwa njia ya Habari Njema akadhihirisha uhai usio na kifo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini sasa imefunuliwa kwa kudhihirishwa kwake Mwokozi wetu, Al-Masihi Isa, ambaye amebatilisha mauti na kuleta uzima na kutokufa kupitia kwa Injili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na sasa inadhihirishwa kwa kufunuliwa kwake Mwokozi wetu Kristo Yesu; aliyebatili mauti, na kuufunua uzima na kutokuharibika, kwa ile Injili;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
na ambayo sasa imeonyeshwa kwetu kwa kuja kwake Kristo Yesu, Mwokozi wetu. Yeye Kristo aliiharibu mauti na kuleta uzima na kutokufa kwenye nuru kwa njia ya Habari Njema.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
lakini sasa imefunuliwa kwetu kwa kuja kwake Mwokozi wetu Yesu Kristo. Yeye amekomesha nguvu za kifo, na kwa njia ya Habari Njema akadhihirisha uzima usio kufa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
lakini imefunuliwa kwetu sasa kwa kuja kwake Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Yeye amekomesha nguvu za kifo, na kwa njia ya Habari Njema akadhihirisha uhai usio na kifo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini sasa imefunuliwa kwa kudhihirishwa kwake Mwokozi wetu, Kristo Yesu, ambaye amebatilisha mauti na kuleta uzima na kutokufa kwa njia ya Injili.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini sasa imefunuliwa kwa kudhihirishwa kwake Mwokozi wetu, Al-Masihi Isa, ambaye amebatilisha mauti na kuleta uzima na kutokufa kwa njia ya Injili.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na sasa inadhihirishwa kwa kufunuliwa kwake Mwokozi wetu Kristo Yesu; aliyebatili mauti, na kuufunua uzima na kutoharibika, kwa ile Injili;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
lakini imefunuliwa kwetu sasa kwa kuja kwake Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Yeye amekomesha nguvu za kifo, na kwa njia ya Habari Njema akadhihirisha uhai usio na kifo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini siku za sasa yametufunikia hapo, mwokozi wetu Kristo Yesu alipotokea; ndiye aliyezitangua nguvu za kifo, kisha akatokeza mwangani uzima usioangamika, kama tulivyoambiwa na Utume mwema;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na sasa inadhihirishwa kwa kufunuliwa kwake Mwokozi wetu Kristo Yesu; aliyebatili mauti, na kuufunua uzima na kutokuharibika, kwa ile Injili;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini neema hii imeonekana sasa kwa kuja kwa Mwokozi wetu Kristo Yesu. Yeye ameshinda nguvu za lufu na kwa njia ya Habari Njema ameonyesha wazi uzima wa milele.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
na sasa inadhihirishwa kwa kufunuliwa kwake Mwokozi wetu Yesu Kristo, aliyebatili mauti na kuufunua uzima ua kutoa kuharibika, kwa ile Injili,