2 Timothy 1:13 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Shika kwa makini mafundisho yale ya kweli niliyokufundisha na kubaki katika hiyo imani na huo upendo wetu katika kuungana na Kristo Yesu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Shika kwa uthabiti kielelezo cha mafundisho yenye uzima uliyoyasikia kwangu, pamoja na imani na upendo katika Al-Masihi Isa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Shika kielelezo cha maneno yenye uzima uliyoyasikia kwangu, katika imani na upendo ulio katika Kristo Yesu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yale uliyoyasikia nikiyafundisha yawe mfano kwako wa mafundisho utakayofundisha wewe. Uyafuate na yawe kielelezo cha mafundisho ya kweli na uzima kwa uaminifu na upendo ule ule ambao Kristo Yesu ametuonesha.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Shika kwa makini mafundisho yale ya kweli niliyokufundisha, na kubaki katika hiyo imani na huo upendo wetu katika kuungana na Kristo Yesu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Shika kwa makini mafundisho yale ya kweli niliyokufundisha na kubaki katika hiyo imani na huo upendo wetu katika kuungana na Kristo Yesu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Shika kwa uthabiti kielelezo cha mafundisho yenye uzima yale uliyoyasikia kwangu, pamoja na imani na upendo katika Kristo Yesu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Shika kwa uthabiti kielelezo cha mafundisho yenye uzima yale uliyoyasikia kwangu, pamoja na imani na upendo katika Al-Masihi Isa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Shika kielelezo cha maneno yenye uzima uliyoyasikia kwangu, katika imani na upendo ulio katika Kristo Yesu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Shika kwa makini mafundisho yale ya kweli niliyokufundisha na kubaki katika hiyo imani na huo upendo wetu katika kuungana na Kristo Yesu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Uliyoyasikia kwangu mimi, shikamana nayo! Kwani ni kielezo cha kujifundishia yale maneno yatupayo uzima, tukimtegemea Kristo Yesu na kumpenda!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Shika kielelezo cha maneno yenye uzima uliyoyasikia kwangu, katika imani na upendo ulio katika Kristo Yesu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ushike maneno ya kweli niliyokufundisha, yapate kuwa mufano kwako. Ushikamane na imani na upendo unaokuwa nao kwa njia ya kuungana kwako na Kristo Yesu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Shika sura ya maneno yenye uzima uliyoyasikia kwangu, katika imani na upendo uiio katika Kristo Yesu.