2 Timothy 1:16 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Bwana aihurumie jamaa ya Onesiforo, kwa sababu aliniburudisha rohoni mara nyingi, wala hakuona haya kwa kuwa nilikuwa kifungoni,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Bwana Isa akawahurumie watu wa nyumbani mwa Onesiforo, kwa sababu aliniburudisha mara kwa mara, wala hakuionea aibu minyororo yangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana awape rehema wale walio wa mlango wake Onesiforo; maana mara nyingi aliniburudisha, wala hakuuonea haya mnyororo wangu;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ninaomba kwamba Bwana ataonesha rehema wa familia ya Onesiforo, amekuwa faraja yangu mara nyingi, na hakuona haya kwa ajili yangu kuwa gerezani.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Bwana aihurumie jamaa ya Onesiforo, kwa sababu aliniburudisha rohoni mara nyingi, wala hakuona haya kwa kuwa nilikuwa kifungoni,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Bwana aihurumie jamaa ya Onesiforo, kwa sababu aliniburudisha rohoni mara nyingi, wala hakuona haya kwa kuwa nilikuwa kifungoni,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Bwana akawahurumie watu wa nyumbani mwa Onesiforo, kwa sababu aliniburudisha mara kwa mara wala hakuionea aibu minyororo yangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Bwana Isa akawahurumie watu wa nyumbani mwa Onesiforo, kwa sababu aliniburudisha mara kwa mara wala hakuionea aibu minyororo yangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Bwana awape rehema wale walio wa jamaa wa Onesiforo; maana mara nyingi aliniburudisha, wala hakuuonea haya mnyororo wangu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Bwana aihurumie jamaa ya Onesiforo, kwa sababu aliniburudisha rohoni mara nyingi, wala hakuona haya kwa kuwa nilikuwa kifungoni,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana awahurumie wao wa nyumbani mwa Onesiforo, kwa kuwa amenipoza moyo mara nyingi; hakuwa na soni ya mafungo yangu,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bwana awape rehema wale walio wa mlango wake Onesiforo; maana mara nyingi aliniburudisha, wala hakuuonea haya mnyororo wangu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Bwana awajalie mema sana watu wa jamaa ya Onesiforo, kwa maana amekuja mara nyingi kunifariji, wala hakusikia haya kwa kuniona niko katika kifungo.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bwana awape rehema walio wa uyumba ya Onesiforo; maana marra nyingi aliniburudisha, wala hakuutahayarikia mnyororo wangu;