2 Timothy 1:3 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ninamshukuru Mungu ambaye ninamtumikia kwa dhamiri safi kama walivyofanya wazee wangu; namshukuru kila ninapokukumbuka katika sala zangu usiku na mchana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ninamshukuru Mungu, ninayemtumikia kwa dhamiri safi kama walivyofanya baba zangu, ninapokukumbuka usiku na mchana katika maombi yangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Namshukuru Mungu, nimwabuduye kwa dhamiri safi tangu zamani za wazee wangu, kama vile nikukumbukavyo wewe daima, katika kuomba kwangu usiku na mchana.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Daima namshukuru Mungu katika maombi yangu ninapokukumbuka usiku na mchana kwa ajili yako. Ni Mungu wa mababu zangu na daima nimemtumikia kwa dhamiri safi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ninamshukuru Mungu ambaye ninamtumikia kwa dhamiri safi kama walivyofanya wazee wangu; namshukuru kila ninapokukumbuka daima katika sala zangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ninamshukuru Mungu ambaye ninamtumikia kwa dhamiri safi kama walivyofanya wazee wangu; namshukuru kila ninapokukumbuka katika sala zangu usiku na mchana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ninamshukuru Mungu, ninayemtumikia kwa dhamiri safi, kama walivyofanya baba zangu, ninapokukumbuka usiku na mchana katika maombi yangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ninamshukuru Mungu, ninayemtumikia kwa dhamiri safi, kama walivyofanya baba zangu, ninapokukumbuka usiku na mchana katika maombi yangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Namshukuru Mungu, nimwabuduye kwa dhamiri safi tangu zamani za wazee wangu, kama vile nikukumbukavyo wewe daima, katika kuomba kwangu usiku na mchana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ninamshukuru Mungu ambaye ninamtumikia kwa dhamiri safi kama walivyofanya wazee wangu; namshukuru kila ninapokukumbuka katika sala zangu usiku na mchana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Namshukuru Mungu, ninayemtambikia tangu siku za baba zangu kwa moyo utakatao kwa kujua mema tu. Nakukumbuka pasipo kukoma nikiomba usiku na mchana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Namshukuru Mungu, nimwabuduye kwa dhamiri safi tangu zamani za wazee wangu, kama vile nikukumbukavyo wewe daima, katika kuomba kwangu usiku na mchana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninamushukuru Mungu ambaye ninamutumikia kwa zamiri safi kama vile babu zangu walivyofanya, ninapokukumbuka siku zote katika maombi yangu usiku na muchana.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Namshukuru Mungu, nimwabuduye tangu zamani za wazee wangu kwa dhamiri safi, kama vile nikukumbukavyo wewe daima, katika kuomba kwangu, mchana na usiku, ninatamani sana kukuona,