2 Timothy 1:7 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa maana Roho tuliyepewa na Mungu si wa kutufanya tuwe waoga; sivyo, ila ni Roho wa kutujalia upendo na nidhamu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Maana Mungu hakutupatia roho ya woga, bali roho ya nguvu, ya upendo na ya moyo wa kiasi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwani Roho ambaye Mungu alitupa sisi ni chanzo cha ujasiri wetu, ni nguvu, upendo na fikra safi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa maana Mungu hakutupa Roho wa kutufanya tuwe waoga, bali alitupa Roho wa kutujalia nguvu, upendo na nidhamu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa maana Roho tuliyepewa na Mungu si wa kutufanya tuwe waoga; sivyo, ila ni Roho wa kutujalia upendo na nidhamu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali roho ya nguvu, ya upendo na ya moyo wa kiasi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali roho ya nguvu, ya upendo na ya moyo wa kiasi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa maana Roho tuliyepewa na Mungu si wa kutufanya tuwe waoga; sivyo, ila ni Roho wa kutujalia upendo na nidhamu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani Mungu hakutupa Roho ya kutuogopesha, ila ya kututia nguvu na upendo tuonyeke.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana Mungu hakutupatia sisi Roho wa kuogopa, lakini Roho anayetupatia nguvu, upendo na kujizuiza.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana Mungu hakutupa roho ya khofu, bali ya nguvu na ya upendo ua ya moyo wa kiasi.