2 Timothy 1:8 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, usione haya kumshuhudia Bwana wetu, wala usione haya kwa sababu yangu mimi niliye mfungwa kwa ajili yake. Lakini shiriki katika mateso kwa ajili ya Habari Njema, kadiri ya nguvu unayopewa na Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo usione haya kushuhudia kuhusu Bwana wetu, wala usinionee haya mimi niliye mfungwa kwa ajili yake. Bali uishiriki pamoja nami taabu ya Injili, kwa kadiri ya nguvu ya Mungu,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi usiuonee haya ushuhuda wa Bwana wetu, wala usinionee haya mimi mfungwa wake, bali uvumilie mabaya pamoja nami kwa ajili ya Injili, kwa kadiri ya nguvu ya Mungu;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo usione aibu kushuhudia juu ya Bwana wetu Yesu au kunionea aibu mimi, niliye mfungwa kwa ajili yake. Bali aliteseka pamoja nami kwa ajili ya Habari Njema na Mungu hutupa nguvu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, usione haya kumshuhudia Bwana wetu, wala usione haya kwa sababu yangu mimi niliye mfungwa kwa ajili yake. Lakini shiriki katika mateso kwa ajili ya Habari Njema, kadiri ya nguvu unazopewa na Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, usione haya kumshuhudia Bwana wetu, wala usione haya kwa sababu yangu mimi niliye mfungwa kwa ajili yake. Lakini shiriki katika mateso kwa ajili ya Habari Njema, kadiri ya nguvu unayopewa na Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo usione haya kushuhudia kuhusu Bwana wetu, wala usinionee haya mimi niliye mfungwa kwa ajili yake. Bali uishiriki pamoja nami taabu ya Injili, kwa kadiri ya nguvu ya Mungu,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo usione haya kushuhudia kuhusu Isa Bwana wetu, wala usinionee haya mimi niliye mfungwa kwa ajili yake. Bali uishiriki pamoja nami taabu ya Injili, kwa kadiri ya nguvu ya Mwenyezi Mungu,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi usiuonee haya ushuhuda wa Bwana wetu, wala usinionee haya mimi mfungwa wake, bali uvumilie mabaya pamoja nami kwa ajili ya Injili, kwa uweza wa Mungu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, usione haya kumshuhudia Bwana wetu, wala usione haya kwa sababu yangu mimi niliye mfungwa kwa ajili yake. Lakini shiriki katika mateso kwa ajili ya Habari Njema, kadiri ya nguvu unayopewa na Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, usiingiwe na soni ya kumshuhudia Bwana wetu, hata mimi niliyefungwa kwa ajili yake! Ila ukiumizwa vibaya kwa ajili ya Utume mwema vumilia pamoja nami kwa nguvu za Mungu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi usiuonee haya ushuhuda wa Bwana wetu, wala usinionee haya mimi mfungwa wake, bali uvumilie mabaya pamoja nami kwa ajili ya Injili, kwa kadiri ya nguvu ya Mungu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, usisikie haya ya kutoa ushuhuda kwa ajili ya Bwana wetu, wala usisikie haya kwa sababu yangu mimi ninayekuwa katika kifungo kwa ajili yake. Lakini ushiriki nami katika mateso kwa ajili ya Habari Njema, kufuatana na uwezo unaopewa na Mungu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi usiutahayarikie ushuhuda wa Bwana wetu, wala mimi mtumwa wake, bali uvumilie mabaya pamoja na Injili kwa kadiri ya nguvu ya Mungu;