2 Timothy 1:9 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yeye alituokoa, akatuita tuwe watu wake yeye mwenyewe, si kwa sababu ya mastahili ya matendo yetu, bali kwa sababu ya kusudi lake na neema yake. Alitujalia neema hiyo kwa ajili ya Kristo Yesu kabla ya wakati,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
ambaye alituokoa na kutuita katika mwito mtakatifu: si kwa kadiri ya matendo yetu mema, bali kwa sababu ya kusudi lake mwenyewe na neema yake. Neema hii tulipewa katika Al-Masihi Isa tangu milele.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ambaye alituokoa akatuita kwa mwito mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu sisi, bali kwa kadiri ya makusudi yake yeye na neema yake. Neema hiyo tulipewa katika Kristo Yesu tangu milele,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Alituokoa na kutuita katika maisha ya utakatifu, sio kwa sababu ya kitu cho chote tulichokifanya wenyewe, bali kwa kusudi lake mwenyewe na neema, ambayo ametupa sisi kwa Kristo Yesu kabla ya mwanzo wa wakati,
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yeye alituokoa, akatuita tuwe watu wake yeye mwenyewe, si kwa sababu ya matendo yetu wenyewe bali kwa sababu ya kusudi lake na neema yake. Alitujalia neema hiyo katika Kristo Yesu kabla mwanzo wa nyakati;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yeye alituokoa, akatuita tuwe watu wake yeye mwenyewe, si kwa sababu ya mastahili ya matendo yetu, bali kwa sababu ya kusudi lake na neema yake. Alitujalia neema hiyo kwa ajili ya Kristo Yesu kabla ya wakati,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
ambaye alituokoa na kutuita katika mwito mtakatifu: si kwa kadiri ya matendo yetu mema bali kwa sababu ya kusudi lake mwenyewe na neema yake. Neema hii tulipewa katika Kristo Yesu kabla ya kuwako kwa ulimwengu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
ambaye alituokoa na kutuita katika mwito mtakatifu: si kwa kadiri ya matendo yetu mema bali kwa sababu ya kusudi lake mwenyewe na neema yake. Neema hii tulipewa katika Al-Masihi Isa tangu milele.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ambaye alituokoa akatuita kwa mwito mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu sisi, bali kwa kadiri ya makusudi yake mwenyewe na neema yake. Neema hiyo tulipewa katika Kristo Yesu tangu milele,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yeye alituokoa, akatuita tuwe watu wake yeye mwenyewe, si kwa sababu ya mastahili ya matendo yetu, bali kwa sababu ya kusudi lake na neema yake. Alitujalia neema hiyo kwa ajili ya Kristo Yesu kabla ya wakati,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Maana ndiye aliyetuokoa, ndiye aliyetuitia kuwa watakatifu; naye hakutuitia kwa hivyo, matendo yetu yalivyo, ila kwa hiyovyo, alivyotaka mwenyewe toka kale kutugawia yale mema yaliyomo mwake Kristo Yesu; ni yayo hayo, tuliyolimbikiwa mbele ya mwanzo wa siku za kale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ambaye alituokoa akatuita kwa mwito mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu sisi, bali kwa kadiri ya makusudi yake yeye na neema yake. Neema hiyo tulipewa katika Kristo Yesu tangu milele,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yeye ndiye aliyetuokoa na kutuita kuwa watu wake, si kwa sababu ya matendo lakini ni kwa sababu ya mupango wake mwenyewe na neema yake aliyotupatia katika kuungana na Kristo Yesu mbele ya nyakati zote.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
aliyetuokoa akatuita kwa wito mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu, bali kwa kadiri ya makusudi yake mwenyewe na neema yake, tuliyopewa sisi katika Kristo Yesu, kabla ya nyakati za zamani;