2 Timothy 2:10 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo navumilia kila kitu kwa ajili ya wateule wa Mungu, ili wao pia wapate ukombozi upatikanao kwa njia ya Yesu Kristo, na ambao huleta utukufu wa milele.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo ninavumilia mambo yote kwa ajili ya wateule wa Mungu, kusudi wao nao wapate wokovu ulio katika Al-Masihi Isa, pamoja na utukufu wa milele.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa ajili ya hilo nastahimili mambo yote, kwa ajili ya wateule, ili wao nao waupate wokovu ule ulio katika Kristo Yesu, pamoja na utukufu wa milele.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa hiyo nayavumilia yote kwa ajili ya wateule wa Mungu, ili na wao waweze kuufikia wokovu unaopatikana katika Kristo Yesu, pamoja na utukufu wa milele.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
na hivyo navumilia kila kitu kwa ajili ya wateule wa Mungu, ili wao pia wapate ukombozi upatikanao kwa njia ya Yesu Kristo, na ambao huleta utukufu wa milele.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo navumilia kila kitu kwa ajili ya wateule wa Mungu, ili wao pia wapate ukombozi upatikanao kwa njia ya Yesu Kristo, na ambao huleta utukufu wa milele.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo ninavumilia mambo yote kwa ajili ya wateule wa Mungu, kusudi wao nao wapate wokovu ulio katika Kristo Yesu, pamoja na utukufu wa milele.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo ninavumilia mambo yote kwa ajili ya wateule wa Mungu, kusudi wao nao wapate wokovu ulio katika Al-Masihi Isa, pamoja na utukufu wa milele.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa ajili ya hilo nastahimili mambo yote, kwa ajili ya wateule, ili wao nao waupate wokovu ule ulio katika Kristo Yesu, pamoja na utukufu wa milele.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo navumilia kila kitu kwa ajili ya wateule wa Mungu, ili wao pia wapate ukombozi upatikanao kwa njia ya Yesu Kristo, na ambao huleta utukufu wa milele.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo nayavumilia yote kwa ajili yao waliochaguliwa, kwamba nao waupate wokovu uliomo mwake Kristo Yesu, wafike penye utukufu wa kale na kale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa ajili ya hilo nastahimili mambo yote, kwa ajili ya wateule, ili wao nao waupate wokovu ule ulio katika Kristo Yesu, pamoja na utukufu wa milele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ni kwa hiyo ninavumilia mambo yote kwa ajili ya watu ambao Mungu alijichagulia kuwa wake, kusudi wao vilevile wapate kuokoka na kupata utukufu wa milele unaopatikana kwa njia ya Kristo Yesu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa ajili ya hilo nastahimili yote, kwa ajili ya wateule, wao nao waupate wokofu ulio katika Kristo Yesu pamoja ua utukufu wa milele.